Saturday, June 15, 2013

Mwanasiasa mkongwe nchini Christopher Mtikila ameshinda kesi aliyofungua Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika (AfCHPR) mjini Arusha akidai Tanzania inakiuka demokrasia inapozuia wagombea binafsi.

Mwanasiasa mkongwe nchini Christopher Mtikila
--- 
Mwanasiasa mkongwe nchini Christopher Mtikila ameshinda kesi aliyofungua Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika (AfCHPR) mjini Arusha akidai Tanzania inakiuka demokrasia inapozuia wagombea binafsi.

Katika hukumu iliyosomwa jana jioni, mahakama imesisitiza kuwa kwa kulazimisha viongozi watoke vyama vya siasa, Tanzania inawanyima wananchi wake fursa huru ya kushiriki kwenye uongozi.
Mchungaji Mtikila, ambaye ana historia ndefu ya kukwaruzana na serikali ya Chama Cha Mapinduzi, alifungua shauri mahakama ya Afrika mwaka 2011 baada ya jitihada zake za kupindua mabadiliko ya kikatiba yaliyofuta ugombea binafsi kugonga mwamba kwenye mahakama za kitaifa.