Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma Deusdedit Nsimeki akipanga maneno ya tembo kulingana na uneno /uzito kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Mwandishi wa habari wa katika Gazeti la Mtanzania Hamoni Mtega akiwa amenyanyua jino la tembo
--------------------------------------------------
JESHI la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kukamata meno ya Tembo
18 yenye uzito wa kilo 84 yenye thamani ya Tsh216,000,000/ambapo meno hayo 18
ni sawa na dola 15 elfu za kimarekani pia ni sawa na Tembo tisa waliouwawa .
Akiongea na waandishi wa habari
ofisini kwake leo Kamanda wa polisi mkoani Ruvuma Deusdedit Nsimeki amesema kuwa tukio hilo la
kukamata meno hayo lilitokea Juni 20 Mwaka huu majira ya saa 3.00 usiku katika
kijiji cha Majala kata ya Nandembo iliyopo wilaya ya Tunduru mkoani
Ruvuma .
Kamanda Nsimeki amesema kuwa tukio hilo la kukamatwa kwa meno hayo ya tembo
lilitokea baada ya askari polisi wa
wilaya hiyo kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema ndipo wao waliweka mtego
wa kuwanasa watuhumiwa hao lakini bahati mbaya watuhumiwa hao walikurupuka na
kuacha mizigo ya meno hayo iliyokuwa imefungwa kwenye mifuko tofauti tofauti.
Alisema kuwa watuhumiwa waliokurupuka walikuwa wanne huku kila mmoja
na baiskeli ambazo walikuwa wamebebea meno hayo na kwa upande wa watuhumiwa wa
meno ya tembo kukurupuka bila kutiwa mbaroni na jeshi hilo limekuwa ni tukio la
pili la kwanza lilitokea katika kijiji cha Hanga wilayani Namtumbo na la
pili ndiyo hilo la wilaya ya Tunduru zote za mkoani Ruvuma .
Aidha kamanda alisema kuwa jeshi la
polisi linajitahidi kuwasaka watu ambao wamejificha na wanajihusha na matukio
hayo ya ujangili kwa wanyama na hasa tembo.
Pia ametoa
wito kwa wananchi uendelea kushirikiana jeshi la polisi mkoani Ruvuma kwa kutoa
taarifa za siri zitakazowezesha kukamatwa kwa wahusika wa vitendo vya uhalifu
wa aina yoyote kwa sababu suala la ulinzi ni kila mmoja hivyo kunasoaswa kuwepo
kwa ushirikiano wa karibu baina ya polisi na wananchi.
VIA/demashonews