Thursday, June 6, 2013

JK amaliza Ziara yake Singapore, Ufundi, mipango miji na uendelezaji bandari vyamvutia


Rais Jakaya kikwete akiendelea kuangalia mfano wa Nchi ya Singapore na kupata maelezo ya jinsi mamlaka inayohusika na mipango miji wanavyodhibiti ujenzi wa makazi ili kuendana na changamoto ya uhaba wa ardhi ya nchi hii ambayo ukubwa wake ni km2 710 tu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakitembezwa kwenye makao makuu ya Mamlaka ya Ustawishaji mijini ya Singapore leo Juni 6, 2013.ambapo wanajionea mfano wa jiji hilo ukiwa umetengenezwa mahususi kwa kuhakikisha mji unapangwa na kusimamiwa kisayansi kwa mipango miji ya muda mfupi na muda mrefu

Baadhi ya wafanyabiashara walioongozana na Rais Jakaya Kikwete katika ziara ya kikazi nchini Singapore wakiwa katika picha ya kumbukumbu na mawaziri walio katika msafara huoleo Juni 6, 2013. . Wa pili kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe akifuatiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda na Waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe (wa tatu) kulia. 
Mojawapo ya vivutio vikubwa katika jiji la Singapore ni hoteli hii ya kitalii na casino iitwayo Marina Bay ambayo kuna jengo la mgahawa  lenye umbo la meli juu ya majengo yake mawili   
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake katika picha ya pamoja na viongozi wa Mamlaka ya Ustawishaji Upya ya Miji ya Singapore leo Juni 6, 2013.  
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakitembelea Taasisi ya Elimu  ya ufundi (Institute of Technical education) iliyo sawa na VETA kwa Tanzania leo Juni 6, 2013.ambapo pamoja na mambo mengine walijionea jinsi wanafunzi wake wanavyofundishwa kuunda vipuli vya aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na vya ndege
Rais Jakaya Kikwete akioneshwa Ndege inayotumiwa kufundisha wanafunzi katika kituo cha mafunzo ya ufundi cha Singapore

PICHA NA IKULU