Saturday, June 8, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, AFUNGUA KONGAMANO LA USHINDANI WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua kongamano kuhusu ushindani kwa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki lililoandaliwa na Jukwaa la Uchumi Duniani (World  Economic Forum) na kufanyika New Arusha Hotel jijini Arusha leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Richard Sezibera (kulia), Mkuu wa mkoa Arusha, Magesa Mulongo (kushoto) na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, wakifuatilia moja ya mada zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye kongamano hilo kuhusu ushindani kwa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki lililoandaliwa na Jukwaa la Uchumi Duniani (World  Economic Forum) na kufanyika New Arusha Hotel jijini Arusha leo.
 Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akiteta jambo na Lawrance Masha, wakiwa katika Kongamano hilo.
 Wajumbe wa kongamano kuhusu ushindani kwa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki lililoandaliwa na Jukwaa la Uchumi Duniani (World  Economic Forum) wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipokua akifungua Kongamano hilo leo katika Hoteli ya New Arusha Hotel jijini Arusha leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika mashariki Richard Sezibera baada ya kufungua kongamano kuhusu ushindani kwa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki lililoandaliwa na Jukwaa la Uchumi Duniani (World  Economic Forum) na kufanyika New Arusha Hotel jijini Arusha leo
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, katikati akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kongamano kuhusu ushindani kwa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais