Wajumbe
wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania(ALAT) Mkoa wa Ruvuma wakikagua
mradi wa vyanzo vya Maji vilivyopo katika mlima Matogoro mjini Songea,
Wajumbe
wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania(ALAT) Mkoa wa Ruvuma wakikagua
mradi wa Kibanio cha umwagiliaji katika kata ya Subila iliyopo Manispaa
ya Songea
Banio hili limegharimu kiasi cha Tshs Milioni Mia mbili ishirini hadi kufikia hapa lilipo.
Wajumbe
wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania(ALAT) Mkoa wa Ruvuma wakiwa
katika kituo kikuu cha mabasi kinachojengwa katika eneo la Msamala kwa
mfumo wa JENGA ,ENDESHA,KABIDHI.
Mfumo
huu unamuwezesha mwananchi kujenga kibanda nakukitumia kwa mkataba wa
miaka kumi na moja kisha anakabidhi halmashauri ya Manispaa ya
Songea.Hata hivyo wajumbe walihoji juu ya ujenzi huo na ukubwa wa eneo
kulingana na ongezeko la watu, magari na huduma nyinginezo katika eneo
hilo kuwa haliwezi kukidhi ongezeko hilo kutokana na eneo hilo kuonekana
dogo.
Wajumbe
wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania(ALAT) Mkoa wa Ruvuma wakiendelea
kuhoji juu ya ujenzi wa kituo hicho kipya cha Mabasi ambacho kimezua
utata miongoni mwa wajumbe hao.
Toka
kushoto ni katibu wa ALAT mkoa wa Ruvuma Mohamedi Maje akiwa na mjumbe
kutoka wilayani Tunduru wakiwa wameshikwa na butwaa baada ya taarifa ya
utekelezaji wa ujenzi wa kituo hicho cha Mabasi
Kaimu
Mhandisi wa Manispaa ya Songea Davis Mbawala akijibu maswali ya
wajumbe juu ya ujenzi wa kituo kipya cha mabasi kinachojengwa kwa mfumo
wa JENGA,ENDESHA,KABIDHI,
Toka
kulia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Songea Wiloni Kapinga, Mwandishi wa
habari wa ALAT mkoa wa Ruvuma Nathan Mtega na mkurugenzi wa Halmashauri
ya Namtumbo ambaye pia ni Katibu wa ALAT mkoa wa Ruvuma Mohamed Maje
wakiwa katika picha ya pamoja
Katibu wa ALAT mkoa wa Ruvuma Mohamed Maje akiteta jambo na Naibu Meya
wa Manispaa ya Songea Wiloni Kapinga wakati wa majumuisho ya ziara ya
wajumbe wa ALAT baada ya ukaguzi wa miradi
Wajumbe wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania(ALAT) Mkoa wa Ruvuma wakiwa ndani ya ukumbi wa mkutano
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru akitoa hoja katika kikao cha majumuisho baada ya ziara ya kukagua miradi
Mwandishi wa habari Cresencia Kapinga akitoa mapendekezo katika kikao cha majumuisho.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Tunduru Robert Nehata akiuliza swali
katibu ALAT Mohamed Maje akizungumza kabla ya kumkaribisha mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho