Mkuu
wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akizungumza kabla ya
kuwakabidhi piki piki tano viongozi wa SACCOS ya waendesha piki piki wa
Manispaa ya Songea.
Wanachama
wa SACCOS ya waendesha piki piki wa Manispaa ya Songea wakimsikiliza
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.alipokuwa akitoa nasaha zake kabla ya kuwakabidhi
piki piki
Mkuu wa Mkoa Ruvuma Said Mwambungu akijaribu kuwasha moja ya piki piki alizozitoa kabla ya kukabidhi.
Mkuu
wa mkoa wa Ruvuma akijaribu kuendesha piki piki kabla ya kuwakabidhi
viongozi wa SACCOS hiyo ya waendesha piki piki wa Manispaa ya Songea.
Mkuu
wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwanbungu akimkabidhi kadi za piki piki hizo
Mwenyekiti wa umoja wa waendesha piki piki wa Manispaa ya Songea Shaban
Kassimu.
Mwenyekiti
wa SACCOS ya waendesha piki piki wa Manispaa ya Songea Shaban Kassimu
akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma baada ya kumkabidhi kadi na piki piki
tano.
Mkuu
wa Mkoa wa Ruvuma wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa SACCOS
hiyo kushoto kwa aliyevaa suti ni Mkuu wa wilaya ya Tunduru Chande
Nalicho, Mkuu wa mkoa Ruvuma Said Mwambungu
Viongozi wa SACCOS ya waendesha Piki piki wakiondoka baada ya kukabidhiwa piki piki
------------------------------------------------------------------
Na Nathan Mtega,Songea
Mkuu wa Mkoa wa
Ruvuma Said Mwambungu amewakabidhi piki piki tano zenye thamani ya shilingi milioni kumi wanachama wa chama cha akiba
na mikopo cha waendesha piki ipiki wa
Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma ikiwa sehemu ya kuwafanya waendesha piki piki
kuweza kujitegemeza na kumiliki piki piki zao badala ya kuendelea kutumiwa na
wamiliki wa piki piki wanaofanya biashara ya kubeba abiria.
Akizungumza kabla ya
kuwakabidhi piki piki hizo mkuu wa mkoa amesema kuwa mara baada ya kufika
mkoani Ruvuma alibaini kuwepo kwa waendesha piki piki wengi wanaofanya biashara
ya kubeba abiria kwa kutumia piki piki ambazo haziwamiliki hali inayowafanya kuendelea
kuwa wategemezi kwa wamiliki wa piki hizo.
Alisema kuwa aliamua kukutana na waendesha piki piki wote wa
Manispaa ya Songea wapatao elfu tatu na kuwataka kuwa na umoja utakaowawezesha
kuanzisha chama cha akiba na mikopo ili waweze kukopesheka kwa ajili ya
kujiinua kiuchumi na kuweza kumiliki piki piki zao badala ya kutumiwa na
wamiliki.
Aidha aliwataka baada ya kujiunga na kuanzisha chama cha
akiba na mikopo wafunguwe akaunti benki ndipo yeye atatoa piki piki tano kwa
ajili ya kuwawezesha kuanza kujitegemeza ahadi ambayo ameitekeleza kwa
kuwakabidhi vionhozi wa chama hicho piki piki hizo huku akiahidi kuwapa piki
piki nyingine muda wowote na kuwataka kuzintunza na kuzitumia kwa uangalifu kwa
sababu ni mali yao wenyewe tofauti na
zile ambazo wamekuwa wakizitumia.
Amesema kuwa uongozi na wanachama wanapaswa kuweka mipango
ya namna ya kuzitumia piki piki hizo ili ziweze kuzalisha piki piki nyingine
kwa ajili ya wengine kwa sababu hizo ni kianzio cha wao kujitegemeza na amesema
kuwa mpango huo wa kuanzishwa kwa vyama vya aikiba na mikopo kwa waendesha piki
piki utaendelezwa kwa wilaya zote za mkoa wa Ruvuma.
Akimshukuru Mkuu wa mkoa kwa niaba ya wanachama wa chama hicho cha akiba na mikopo cha waendesha piki
piki wa Manispaa ya Songea mwenyekiti wa chama hicho Shaban Kassimu alisema
kuwa piki piki hizo zitawasaidia wanachama hao kuboresha maisha yao na
kujikwamua kiuchumi pamoja na kupunguza
utegemezi uliokuwepo.
Alisema kuwa utawekwa utaratibu mzuri wa kuzitumia piki hizo
ili ziweze kuzalisha na kuwakopesha wengine ambao watakuwa wamejiunga kwenye
chama hicho pia zitawasaidia waendesha piki piki kuzingatia sheria za usalama bara
barani kwa sababu ni mali yao wenyewe tofauti na ilivyokuwa awali hawakuwa na
uchungu kwa sababu hazikuwa mali yao.
Mwisho
VIA/ demashonews
VIA/ demashonews