Tuesday, June 4, 2013

BREAKING NEWS : Wachinjaji wa ng'ombe Songea watangaza mgomo

Issa Bakari ama Mr. Big alizungumza kwa niaba ya wachinjaji  wa songea kufuatia kubomolewa kwa mazizi ya kuhifadhia ng'ombe.
Mwenyekiti wa umoja wa wachinjaji wa ng’ombe wa Manispaa ya Songea ambaye pia ni diwani wa kata ya Misufini Salum Mfamaji akitoa kero zake kwa waandishi wa habari waliojitokeza katika tukio hilo usiku huu.
Diwani wa kata ya Msamala Bw.Mgwasaakizungumza na wafanya biashara kutafuta muafaka ili kuepuka madhara ambayo yanaweza kujitokeza kwa kesho kutokana na mgomo huo
Huu ni umati uliuokusanyika wa wachinjaji wa ng’ombe pamoja na wamiliki na wafanyabiashara wa Manispaa ya Songea wakijadili kubomolewa mazizi yao
Hawa ni ng'ombe ambao wamebomolewa mazizi  yao na sasa wametapakaa katika uwanja na kuwafanya wafanyabiashara  kukesha usiku huu kwa kuwalinda ili waipotee na kusababisha hasara
...................................................
Na Nathan Mtega,Songea
 
 WAKAZI  wa mji wa Songea mkoani Ruvuma wako hatarini kukosa kitoweo cha nyama ya ng’ombe kufuatia mgomo uliotangazwa na wachinjaji hao wa ng’ombe pamoja na wamiliki na wafanyabiashara baada ya mazizi ya kuhifadhia mg’ombe yaliyopo katika machinjio ya kata ya Msamala mjini Songea kuvunjwa kwa amri ya uongozi wa halmashauri ya Manispaa ya Songea bila wao kujulishwa kuhusisana na hatua hiyo.
 
 Wakizungumza na waandishi wa habari wachinjaji hao zaidi ya mia mbili muda mfupi baada ya tukio hilo la kuvunjwa kwa mazizi hayo ya machinjio wakiongozwa na Issa Bakari walisema kuwa kulikuwa na mpango wa uongozi wa halmashauri ya Manispaa ya Songea kuhamisha machinjio hayo na kuyapeleka katika kata ya Tanga kwenye kitongoji cha Masigila ambao ulikuwa bado haujaanza kutekelezwa.
 
 Akizungumza Issa Bakari kwa niaba ya wachinjaji wenzake alisema kuwa eneo hilo ambalo linaelezwa na uongozi wa Manispaa kuwa ndiko ambako wachinjaji wanapaswa kuhamishiwa kwa shughuli hizo bado hakujaandaliwa na hakuna miundo mbinu ya kukidhi ikiwemo vyoo pamoja na mazingira ya kuwatunzia ng’ombe hao kabla ya kuchinjwa.
 
 Alisema kuwa wao hawajakataa uamuzi huon lakini walipaswa kushirikishwa kwa kila hatua ya utekelezaji badala ya kuvunja mazizi huku ng’ombe wakiwepo na hawajui hatma ya ng’ombe wao ambao hawatakuwa na msahali pa kuhifadhiwa kabla ya kuchinjwa na tukio hilo limefanywa usiku wa Juni 4 majira ya saa 1;30 usiku bila taarifa.
 
 Akizungumza diwani wa kata ya Msamala Bw.Mgwasa alisema kuwa yeye ni miongoni mwa madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Songea lakini hakuna kikao kilichoketi na kufikia maamuzi hayo ya kuvunja mazizi hayo hali ambayo inapaswa kulaaniwa na kila mmoja huku akiwasihi wachinjaji hao kutositisha huduma hiyo muhimu kwa wananchi na suala hilo litafanyiwa kazi kazi mara moja na kutadutiwa ufumbuzi bila kuwaathiri wafanyabiashara hao pamoja na wananchi kwa ujumla.
 
 Naye mwenyekiti wa umoja wa wachinjaji wa ng’ombe wa Manispaa ya Songea ambaye pia ni diwani wa kata ya Misufini Salum Mfamaji mbali ya kusisitiza kuwa huenda huduma hiyo ikasitishwa kuanzia kesho lakini aliwaomba wachinjaji hao kuwa na subira wakati viongozi wao wakiendelea kutafuta ufumbuzi kwa kufuata taratibu za halmashauri ya Manispaa ya Songea.
 
VIA/ Demashonews.blogspot.com