Monday, June 10, 2013

Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal Akutana Kwa Mazungumzo na Mhariri wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri Mtendaji wa New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda IKULU Jijini Dar es Salaam Leo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mhariri wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri Mtendaji wa New Habari (2006) Ltd, AbsalomKibanda, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa mazungumzo. Kibanda alimtembelea Mhe. Makamu ili kumwelezea hali yake kiafya inavyoendelea baada ya matibabu.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais