Waziri wa mambo ya ndani Dr. Emmanuel Nchimbi akimkabidhi medali mwakilishi wa mauzo wa kampuni ya ASAS DAIRIES Bw Jimmy kiwelu
Waziri wa mambo ya ndani Dr. Emmanuel Nchimbi akipata maelezo juu ya bidhaa za kampuni ya ASAS DAIRIES wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya washiriki
Kutokana na ubora wa bidhaa hizo hapo ni mteja ambaye ameamua kuja na boksi iliafungiwe mzigo
Huduma zinaendelea na wateja wanafurahia bidhaa za ASAS DAIRIES
.................................
Katika maonyesho ya wiki ya kunywa maziwa kitaifa yaliyo fanyika mkoni Ruvuma 29 may na kumalizika 1 june 2013 katika viwanja vya manispaa Songea , Kampuni ya usindikaji bidhaa za maziwa ya ASAS DAIRIES ya mkoani IRINGA imejinyakulia medali tano (5) mbili za dhahabu , moja ya fedha , moja ya ushiriki na moja ya ushindi wa jumla ,
Maonyesho hayo yaliandaliwa na Tanzania Dairies Board (TDB) kwakushirikiana na Tanzania Milk Processors Association (TAMPA).
Maadhimisho ya wiki ya maziwa yalianza 29 May na kufunguliwa na mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu na kuhitimishwa na Waziri wa mambo ya ndani Dr Emmanuel Nchimbi tarehe 1 June 2013
Katika maonyesho hayo Makampuni na wajasiriamali kadhaa wanaojihusisha na usindikaji wa bidhaa za maziwa walishindanisha bidhaa zao kwa upande wa makampuni makubwa yaliyoshiriki maonyesho hayo ni Tan Dairies ya Dar es salaam,Tangafresh ya Tanga,Engiten ya Arusha, Cefa ya Njombe na Asas Dairies ya Iringa.
Kwaupande wa vikundi vingine ni Nronga group ya Kilimanjaro, kalali group ya kilimanjaro Jitume, uvingo group, Agape group,Profet investiment. Victoria Maziwa mara, fukeni mini dairies, viwawa Cooperatives na Inuka groupe.
Asas Dairies Ilishinda kwa kutwaa gold medal kadhaa pamoja na kuwa mshindi wa jumla wa maonyesho hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari mwakilishi wa kampuni ya Asas dairies kwa nyanda za juu kusini Bw.Jimmy Kiwelu kwanza aliwashukuru wananchi wa mkoa wa Ruvuma kwa mwitikio walio uonyesha kwa kujitokeza kwa wingi katika maonyesho ya wiki ya maziwa kitaifa pia kwa kupenda bidhaa za Asas dairies
“ Wakati tunakuja tulichukua bidhaa kidogo kwani hatukuwa na mategemeo kama mwamko ungekuwa mkubwa kiasi hiki kwa kupenda zaidi bidhaa zetu kuliko za makampuni mengine yaliyoshiriki katika maonyesho ya wiki ya maziwa na baada ya kuona hivyo ilitulazimu kuleta shehena nyingine ya bidhaa “ alisema.
JIMMY ameendelea kusema baada ya kugundua soko hili kwa sasa kampuni ya Asas dairies ltd inampango wa kufungua sales depot ambapo wateja wao watakuwa wanajipatia bidhaa za Asas Dairies kiurahisi hapahapa Songea mjini kuliko hapo awali walikuwa wanatumiwa toka Iringa