Saturday, June 1, 2013

Deo Philikunjombe Nyota yake yang'ara Ludewa

Pichani ni Gari la wagonjwa la Mlangali ambalo limetolewa na Mbunge Deo Philikunjombe


Hivi Karibuni nimetembelea jimbo la Ludewa ambako Mbunge wake ni Deo Philikunjombe, Kijana aliyotokea katika fani ya uandishi wa Habari. Nimefurahishwa sana na jinsi anavyokubalika kwa wananchi ambao ndio waajiri wake na ndio wapiga kura wake.

Nimefurahishwa pia na jinsi anavyochangia maendeleo ya wananchi na jinsi anavyowapigania kuhakikisha miundombinu inaboreshwa, madini ya Chuma na Makaa ya mawe yanawanufaisha wananchi, huduma za afya zinaboreshwa ikiwemo mchango wake binafsi wa Magari ya wagonjwa, vikundi vya SACCOS, Maji nakadharika. Big Up Deo Mpiganaji.

Pichani ni Mwambao wa ziwa Nyasa katika eneo la Lupingu ambako barabara ya kufika huko inatengenezwa kuanzia mwaka ujao wa fedha.

Deo Philikunjombe pia ametoa mchango Mkubwa kupigania usafiri wa Majini katika Mwambao wa ziwa Nyasa na sasa Serikali ipo mbioni kujenga meli moja katika ziwa Nyasa kwa ajili ya kusaidia usafiri wa Majini.