Na
James Gashumba, EANA
Makadirio
ya bajeti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) iliyowasilishwa mwishoni mwa
wiki kwa mwaka wa fedha wa 2013/2014 imepunguza matumizi yake kwa dola za
Kimarekani zipatazo milioni 10 kwa kulinganisha na matumizi ya mwaka
uliopita.
Makadirio
ya bajeti kwa mwaka ujao wa fedha umefikia dola za Kimarekani milioni 130.4
kutoka dola milioni 140 za mwaka wa fedha wa 2012/2013,Shirika la Huru la
Habari la Afrika Mashairki (EANA) limeripoti.
Mwenyekiti
wa Baraza la Mawaziri wa EAC ambaye pia ni Waziri wa Nchi anayeshugulikia
Masuala ya EAC Uganda, Shem Bageine,aliwasilisha makadirio ya bajeti hiyo kwa
Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA) linaloketi mjini Kampla, Uganda,
juzi huku likitoa misisitizo wa utekelezaji wa itifaki ya Soko la Pamoja.
Jumuiya
hiyo imetenga dola milioni 2.2 kwa ajili ya usalama wa chakula katika kanda
hiyo na uhifadhi wa mazingira, hususani ya ziwa Victoria, kwa mujibu wa
Bagaine.
Kiasi
kipatacho dola milioni 30 zitatumika katika shughuli mbalimbali za Kamisheni ya
Bonde la Ziwa Victoria.
Maeneo
mengine yaliyopewa kipaumbele katika matumizi hayo ni pamoja na mpango kabambe
wa mabadiliko ya tabia nchi na viwanda vya kuongeza ubora wa bihaa zitokanazo
na kilimo.
Katika
makadirio ya bajeti yote, Sekretarieti ya EAC itapewa dola za Kimarekani
milioni 69.8,EALA dola milioni 13.1 na Mahakama ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki(EACJ) imetengewa dola milioni 4.3.
Nalo
Baraza la Vyuo Vikuu la Afrika Mashariki litapatiwa dola za Kimarekani milioni
9.7 huku dola milioni 3.2 zimetengwa kwa ajili ya Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa
Victoria.
Bageine
aliliambia bunge hilo kuwa msisitizo mkubwa utawekwa kwenye utekelezaji wa
vipengele vya uhuru wa upatikanaji wa ajira miongoni mwa nchi wanachama pamoja
na mtangamano wa masoko ya fedha ili kuruhusu uhamishaji wa mitaji.
Jumuiya
hiyo pia imepanga kujikita katika kuimarisha itifaki ya Soko la Pamoja na
kuhitimisha majadiliano juu ya kuelekea kwenye Itifaki ya Umoja wa Fedha.