Binti mmoja aliyefahamika kwa jina la Khadija Idd
anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Morogoro akidaiwa kumtupa barabarani
mtoto wake mwenye umri wa miezi 6 baada ya mwanaume aliyezaa naye
kumkataa.
Shuhuda
wetu ambaye ni dereva wa bodaboda aliyefahamika kwa jina la Shabani,
alisema tukio hilo lilitokea Juni 11, mwaka huu maeneo ya Mafiga karibu
na Msikiti wa Mahita ambapo Khadija alichukua uamuzi huo baada ya
mwanaume aliyezaa naye kumgomea mtoto kwa madai ana nywele za Kiarabu
hivyo si wake.
“Huyu dada alifika kwenye kijiwe chetu akiwa amembeba mtoto mgongoni na kukodi pikipiki ili nimpeleke mjini.
“Tulipofika
kwenye msitu uliopo karibu na mashamba ya SUA, aliniambia niendeshe
spidi kuna mtu anamuwahi.
Nilitii amri lakini tulipofika mbele kidogo nikashangaa anamtupa yule mtoto.
Nilitii amri lakini tulipofika mbele kidogo nikashangaa anamtupa yule mtoto.
“Nilipoona
vile nilisimama na kumhoji kwa nini anafanya vile, akawa hajibu.
Nikamchukua na kumpeleka kituo kikuu cha polisi akiwa hana mtoto. Baadae
wasamaria wema walimuokota mtoto akiwa ameumia na kumfikisha polisi,”
alisema mtoa habari huyo.
Mwandishi
wetu alifika katika kituo hicho cha polisi na kufanikiwa kumkuta
Khadija akiwa chini ya ulinzi mkali huku mwanaye akitokwa na damu usoni
na alipoulizwa kulikoni alisema:
“Jamani naomba msamaha, nimefanya
hivyo kwa hasira baada ya baba wa mtoto kudai si wake, eti ni Mwarabu
wakati yeye ni Mngoni wa Songea, nisameheni sitarudia tena.”
Akizungumza
na mwandishi wetu, Kaimu Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Morogoro, Tausi
Mbalamwezi alisema mwanamke huyo amefanya kitendo kibaya na sasa
wanamsaka baba wa mtoto ili amlee huku mtuhumiwa akisuburi taratibu
nyingine.
“Yupo hapa na tumemkuta na kadi ya kliniki ikionesha kuwa,
baba wa mtoto anaitwa Costa Haule. Huyu hana nia njema na mtoto kwani
alitaka kumuua kwa hiyo baada ya kumtibia tunawatafuta ndugu wa mwanaume
au baba wa mtoto ili wamlee wakati tukiandaa utaratibu wa kumfikisha
mahakamani,” alisema Afande Tausi.
GPL