Jackson Odoyo,Dar es Salaam
KESI inayomkabili aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC1), Jerry Murro na wenzake wawili,Edmund Kapama maarufu kama ‘Dokta’ na Deogratius Mugassa imeingia utata baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kusitisha kusikiliza kesi hiyo ili kuipa Jamhuri nafasi ya kukataa rufaa upya.
Jamhuri inapinga kesi hiyo kusikilizwa kama rufaa badala yake inataka ianze upya kwa sababu hukumu iliyotolewa mwaka 2011 na Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Frank Moshi ilikuwa na makosa.
Hata hivyo katika Hukumu hiyo Hakimu Moshi alisema kwamba upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka dhidi ya washitakiwa bila kuacha mashaka yoyote,hata hivyo upande wa Jamhuri ulipinga hukumu hiyo nakukata rufaa Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam.