Monday, June 3, 2013

MAREHEMU ALBERT MANGWEA AAGWA NCHINI AFRIKA KUSINI. MWILI WAKE KUWASILI KESHO NCHINI.

 Watanzania waishio nchini South Africa
wamepata nafasi ya kuaga mwili wa Albert Mangweha
 kuelekea katika safari ya mwisho. Shughuli hiyo imeongozwa na msanii
Bushoke pamoja na Kinjeketile Mwiru.

Baadhi ya watanzania waishio Afrika Kusini wakitoa heshima ya mwisho kwa marehemu Albert Mangwea
Kinjekitile (katikati) akiwa na baadhi ya watanzania waliohudhuria shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu Mangwea
Msanii Bushoke akiwa na moja wapo wa wadu nchini Afrika Kusini wakati wa shughuli ya kumuaga mpendwa wetu Albert Mangwea
Wadau wa Sauzi wakiwa katika harakati za kuusafirisha mwili wa msanii wa kizazi kipya aliyefariki majuzi marehemu  Albert  Mangwear jioni hii huko  Johannesburg, Afrika Kusini. Ratiba zinaonesha mwili huo utawasili kesho jijini Dar es salaam. Muda na ratiba kamili zitafuata punde