Tuesday, June 11, 2013

KAMPUNI YA VODA COM TANZANIA YAZINDUA MRADI WA MWEI (M-PESA WOMEN EMPOWERMENT INITIATIVE – SONGEA MKOANI RUVUMA

 Mkuu wa Wilaya Songea Joseph Mkirikiti akizungumza na akina mama wajane wa Manispaa ya Songea wakati wa uzinduzi  wa mradi wa MWEI (M-Pesa Women Empowerment Initiative) katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa wilaya
 Meneja wa Voda Com Fonundation Mwamvua Mlangwa akimpa maelekezo namna ya kujaza fomu za maombi ya mkopo Grace Kienyi mkazi wa kata ya Lilambo
 Washiriki wakijaza fomu za maombi ya mkopo
Kutoka kushoto ni Meneja wa Voda Com Fonundation Mwamvua Mlangwa akiteta jambo na Meneja mawasiliano wa Voda Com Rukia Mtingwa
 Mwandishi wa habari wa kituo cha ITV mkoa wa Ruvuma Bw. Nathan Mtega akisalimiana na Meneja mawasiliano wa Voda Com Rukia Mtingwa wakati wa uzinduzi wa mradi wa MWEI (M-Pesa Women Empowerment Initiative) mkoani Ruvuma.
Hawa ni miongoni mwa mama wajane waliojitokeza wakisikiza kwa makini maelekezo ya mkopo wa mradi wa MWEI (M-Pesa Women Empowerment Initiative)
 Meneja wa Voda Com Fonundition Mwamvua Mlangwa akiwaelezea akina mama wajane  masharti ya mkopo wa mradi wa MWEI (M-Pesa Women Empowerment Initiative)
Meneja mawasiliano wa Voda Com Rukia Mtingwa akijaribu kuwafafanulia maana halisi ya neno mjasiriamali kwa akina mama wajane ambao ni wajasiriamali waliohudhulia katika uzinduzi wa mradi wa MWEI (M-Pesa Women Empowerment Initiative) 
---------------------------------------------------------
Kampuni ya VodaCom Tanzania Limited kupitia kitengo chake cha huduma kwa jamii(Voda Com Fonundation) imebuni mradi wa MWEI (M-Pesa Women Empowerment Initiative) unaotumia huduma ya mpesa kuwapatia mikopo isiyo na riba akina mama wanaoishi katika maeneo ya vijiji.

Mradi huu ni mkakati wa kampuni ya Vodacom katika kusaidia juhudi za Serikali za kupiga vita umasikini hapa nchini. Mradi wa MWEI unalenga kuwaongezea  uwezo wa kiuchumi (Mitaji) akina mama wanaojishuhulisha na shughuli mbali mbali kwa lengo la kujipatia kipato.

Naye Meneja wa Voda Com Fonundition Mwamvua Mlangwa akisoma risala amesema mradi huu ulizinduliwa rasmi na Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Kayanda Pinda mwezi Julai 24. 2011 ambapo mpaka sasa umeshawafikia wakina mama zaidi ya 7000 Tanzania Bara na visiwani.

Kwa upande wa mkoa wa Ruvuma katika bajeti ya mwaka huu mradi huu unatarajia kuwanufaisha  akina mama 400 katika vijiji vya Peramiho, Muhukulu na Kigonsera.

 Akizungumza kabla ya kuzindua mradi huo Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti mbali ya kuishukuru kampuni hiyo ya simu za mkononi kwa kuwakumbuka akina mama wajasiriamali ambao ni walezi wakubwa wa familia lakini pia aliwaasa akina mama hao kuitumia fursa hiyo ipasavyo.

Pia amesema kuwa zipo taasisi na kampuni mbalimbali ambazo zimekuwa zikitoa mikopo huku ikiwa na mashariti magumu, riba pamoja na gharama za uendeshaji ambayo yamekuwa hayatoi fursa kwa baadhi ya makundi wakiwemo akina mama lakini imekuwa tofauti kwa kampuni ya simu ya mkononi ya voda Com kwa kupitia mradi huu wa kuwajengea uwezo akina mama wajasiliamali bila masharti magumu wala riba.


Aidha amesema kuwa serikali ya wilaya itahakikisha kuwa programu hiyo inakuwa endelevu kwa ajili ya kuwanufaisha akina mama wajasiliamali ambao ndiyo nguzo ya familia zao ambazo wanazilea bila kujali itikadi za kisiasa wala imani za kidini.