Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti akiongea kwa msisitizo ofisi juu ya mgogoro
ulijitokeza baina ya wachinja ng'ombe na wauzaji hapani ofisini kwake alipokuwa akiongea na waandishi wa habari
Aliyenyoosha kidole ni Issa Bakari akionyesha banda lililobomolewa na Afisa mifugo wa manispaa ya Songea
Hawa
ni wachinjaji wa ng'ombe wakiwemo wauzaji wa ng'ombe wakiwa katika hali
ya majonzi baada ya kuvunjiwa banda la kuhifadhia ng'ombe kabla ya
kuchinja
Waandishi
wa habari wakimuoji Afisa mifugo mkoa wa Ruvuma Bw. Mwaiganju
aliyesimama katikati ni mwandishi wa habari wa ITV Bw. Nathan Mtega ,
anaefuata ni mwandishi wa habari wa radio Jogoo Millan na alieshikilia
kamera ni Demasho
Hawa ni baadhi ya ng'ombe ambao wapo uwanjani baada ya kuvunjwa banda
..........................................................
MGOGORO umeibuka baina ya wachinjaji na wauzaji wa ng’ombe
wa Manispaa ya Songea dhidi ya baadhi ya watumishi wa idara ya mifugo wa
Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma ambao umesababisha wachinjaji na wauzaji wa ng’ombe
kuitisha mgomo usio na muda maalumu mpaka ufumbuzi wa
tatizo hilo ambalo walidai ni la muda mrefu upatikane.
Mgogoro huo ambao ulianza Juni 4 mwaka huu majira ya saa
12.30 jioni na kudumu mpaka majira ya saa 2 usiku mwenyekiti wa umoja wa
wachinjaji wa ng’ombe wa Mmkoa wa Ruvuma
Salum Mfamaji ambaye pia ni diwani wa
kata ya Misufini alipotangaza kusitisha
huduma hiyo mpaka hapo ufumbuzi wa tatizo hilo ambalo lilikuwa liliwataka wachinjaji
na wauzaji wa ng’ombe kuondoka katika eneo hilo na kwenda kufanyia shughuli zao
katika kata ya Tanga ambako wao walidai hakujaandaaliwa.
Akizungumza kwa niaba
ya wachinjaji Issa Bakari alisema kuwa wao kama wachinjaji hawajakaidi uamuzi
wa Manispaa ya Songea kuhamia katika eneo hilo jipya lakini walishaomba eneo
hilo lifanyiwe marekebisho muhimu ikiw ni pamoja na kuweka miundo mbinu muhimu ikiwemo vyoo na maji kwa ajili ya usalama wa
kiafya kwao na watu wengine watakaokwenda katika eneo hilo kwa ajili ya kupata
huduma hiyo muhimu.
Alisema kuwa tangu
kulipotokea mabadiliko ya watumishi katikas halmashauri ya Manispaa ya Songea
na hasa katika idara ya mifugo kumeibuka na vitendo vya unyanyasaji kwa
wachinjaji vinavyofanywa na baadhi ya watumishi wa idara hiyo ikiwa ni pamoja
na kitendo cha kuamua kuvunja zizi la kuwafadhi ng’ombe kabla ya kuchinjwa
kitendo ambacho kimefanywa bila kutolewa taarifa kwa wachinjaji na wao wameamua
kusitisha huduma hiyo kwa jamii.
Baada ya mjadala wa muda
mrefu diwani wa kata Msamala eneo ambalo
machinjio yapo Sharif Mgwasa alipowaomba wachinjaji hao kuendelea kutoa
huduma hiyo muhimu kwa jamii wakati uongozi ukiendelea na mazungumzo ya kutafua
ufumbuzi wa tatizo hilo lililojitokeza ikiwa ni pamoja na kujua aliyeamuru
kuvunjwa kwa zizi hilo bila kuzingatia utaratibu wa ushirikishwaji wa
wachinjaji’wauzaji na uongozi wa
Manispaa hiyo.
Hata hivyo wachinjaji hao waliendeleakusisitiza kuwa hawako
tayari kuendelea na huduma hiyo mpaka hapo ufumbuzi wa tatizo hilo utakapopatikana
hali iliyoendelea mpaka Juni 4 mwaka huu majira ya saa 2 asubuhi walipoamua
kuanza kuchinja ingawa ni ng’ombe wachache waliochinjwa kwa sababu ya
sintofahamu hiyo iliyotokea huku eneo hilo la machinjio likitawaliwa na vurugu
zilizosababisha askari polisi kufika eneo hilo na kutuliza ghasia hizo.
Naye Mkuu wa wilaya
ya Songea Joseph Mkirikiti akizungumzia hali hiyo iliyojitokeza alisema kuwa
hiyo imetokana na kutokwepo kwa ushirikishwaji wa pande zote zinazohusikia
lakini pia suala la kuvunja zizi hilo haliafiki ni si utaratibu wa busara kwa
sababu ni kitendo cha kihuni na hakipaswi kufumbiwa macho kwa sababu wachinjaji
na wafugaji walipaswa kuandaliwa mazingira mapya ya kufanyia shughuli zao na
suala la kuwahamisha lingefuata.
Hata hivyo ufumbuzi wa sintofahamu hiyo unatarajiwa kufikiwa
kesho kwa kuzikutanisha pande zote kwenye ofisi ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya
Songea
Mwisho.
VIA/www.demashonews.blogspot.com