picha sio ya tukio halisi
Na
Steven Augustino, Tunduru
Imebainishwa kuwa Mahusiano mabaya kati ya
Walimu na Wanafunzi na
Wanafunzi wadaiwa kukataa kukaa katika mabweni
na Hosteli ni miongoni
mwa vikwazo vya maendeleo ya elimu Wilayani
Tunduru Mkoani Ruvuma na
kupelekea Wilaya hiyo kupata matokeo mabaya
kwa wanafunzi waliofanya
mitihani ya Kidato cha pili na cha nne katika
kipindi cha mwaka 2011/2012 .
Hayo yalibainishwa na afisa elimu Sekondari Mwl.
Ally Mtamila wakati
akiwasilisha taarifa ya matokeo ya kidato cha
pili na cha Nne
katikakipindi cha mwaka 2011/2012,
Kwa
mujibu wa tarifa hiyo mwaka 2011 matokeo ya Kidato cha pili Wilaya
hiyo ilifaulisha kwa wastani wa asilimia 35%,
huku takwimu hizo kwa
upande wa matokeo ya Kidato cha Nne katika
kipindi cha mwaka 2012
zikionesha kuwa Wilaya hiyo ilifaulisha kwa
wastani wa asilimia 59.46%
kiwango kilichodaiwa kuwa ni kidogo na
kiliifanya Wilaya yao kushika
nafasi ya mwisho kimkoa.
Awali aikifungua Mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya
Tunduru Chande Nalicho
pamoja na kubainisha kuwa pamoja na serikali
kuwa na vipaumbele
vingine vya maendeleo lakini Elimu ni muhimu
ilikujiletea mabadiliko
ya kweli.
Dc nalicho aliendelea kueleza kuwa Ili
kuwaletea maendeleo wananchi wa
Tunduru ni lazima wilaya ijikite katika
kusimamia elimu na kuhalalisha
uwepo wao na kwamba wasipo wakazania kusomaa
shule maendeleo
yanayopiganiwa na serikali hayatakuwa na maana
yoyote kwao.
Katika taarifa hiyo Mkuu Dc. Nalicho akatolea
mfano wa Takwimu za
ufaulu wa wanafunzi 2764 waliochaguliwa
kujiunga na masomo ya
sekondari
hadi mwishoni mwa mwezi wa tatu ni asilimia 60% ya watoto
wote waliochaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari.
Akizungumzia upande wa Shule za Msingi Mwaka 2011Shule ya Msingi
Nakapanya ilifaulisha Watoto 26 lakini takwimu
zinaonesha kuwa watoto
wote hawakwenda shule na kuongeza kuwa hali
hiyo inawakatisha tama
hata walimu wa shule za msingi zinazofaulisha
watoto hao .
Wakichangia kwa nyakati tofauti Mwl. Issa
Ngajime alisema kuwa chanzo
cha kushamiri kwa utoro,uchangiaji hafifu wa
chakula mashuleni na
wanafunzi kukataa kukaa katika hostel
zilizojengwa katika shule zao
Viongozi wa serikali za Vijiji wanasitahili
kubeba lawama huku
wakiwataka viongozi kutochanganya elimu na
Siasa kwa kuboresha mbinu
za kufundishia na kuchukua hatua kwa Wanafunzi
ambao wamekuwa
wakibainika kuchaguliwa wakiwa hawajui
kusoma,kuandika na kuhesabu.
Mkuu wa shule ya Mgomba Mwl. Elis Banda
alisema kuwa tatizo wanafunzi
kukataa kukaa katika Hosteli linatokana na
kuwepo kwa idadi kubwa ya
watoto wanaosoma katika shule hizo kuwa ni
wakazi wa maeneo husika na
akapendekekeza kuwepo kwa utaratibu wa kutenga
Shule za kanda kwa
ajili ya kupeleka wanafunzi kutoka maeeneo
tofauti huku akiitaka
serikali kutoa maelekezo ya vitabu vya
kununuliwa tofauti na sasa
ambapo kumekuwa na maelekezo ya kuwataka wakuu
wa shule kutumia vitabu
kutoka katika kampuni ya EMACK ambapo alishauri kupunguzwa kwa idadi
ya vitabu vya kufundishia.
Wadau hao waliendelea kubainisha vikwazo
vingine kuwa ni paomja
Na wanafunzi kubeba mimba wakiwa shuleni.
Mkuu
wa Shule ya sekondari Lukumbule Mwl. Mathias Katto akabainisha
vikwazo vingine kuwa shule zao kutokuwa na
walimu wa masomo ya
Sayansi,Shule kutokuwa na maktaba,Watoto
kutoka katika maeneo husika
na miundombinu ya Nyumba wanazo ishi nimbovu ,mila
na destuli potofu
za kuwafundisha watoto wadogo hasa wakike
mafunzo ya kuishi kiunyumba
ambayo hutolewa kupitia mafunzo ambayo
hutolewa katika jando, Unyago
na Msondo na ngoma ya Sakamimba hali ambayo
imekuwa ikipelekea baadhi
ya wanafunzi kuishi kwa wanaume huku wakiwa
wanaendelea na masomo.