Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza
--
KILIMO KUTUMIA SHS. 328,134,60 8,000 KATIKA MWAKA WA FEDHA UJAO
|
Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika inatarajia kutumia jumla ya shilingi 328,134,608,000/- katika mwaka ujao wa fedha.
Takwimu
hizo zimetolewa leo mjini Dodoma na Waziri wa Kilimo, Chakula na
Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza wakati akiwasilisha Bungeni
Makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2013/14.
Alisema
kuwa kati ya fedha hizo, Shilingi 247,094,320,000 ni kwa ajili ya
Matumizi ya kawaida na Shilingi 81,040,288,000 ni kwa ajili ya Matumizi
ya maendeleo.
Chiza aliongeza kuwa Shilingi 210,175,943,000 ni kwa ajili ya Matumizi Mengine (OC) kwa ajili ya Wizara hiyo .
Aidha
,shilingi 25,602,969,000 ni kwa ajili ya Mishahara (PE) ya Wizara na
Shilingi11,315,408,000 ni Mishahara (PE) ya Bodi na Taasisi zote
zilizoko chini ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.
Kwa
upande shughuli za maendeleo, Chiza alisema kuwa Wizara hiyo imetenga
kiasi cha shilingi 23,927,000,000 ikiwa ni fedha za ndani na
shilingi 57,113, 288,000 ni fedha za Nje.
Wabunge
wanatarajia kujadili bajeti ya Wizara ya Kilimo , Chakula na Ushirika
kwa kipindi cha siku mbili ambapo itahitimishwa kesho.
Katika
hatua nyingine Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mhe. Chiza amesema
Serikali inatarajia kufufua Kituo cha Kilimo Anga ili kukiwezesha kuwa
na ndege na Wataalam watakaosaidia kudhibiti milipuko ya visumbufu vya
mazao hasa Nzige.
Mhe.
Chiza amesema kwa kiasi kikubwa Serikali imekuwa ikitegemea huduma ya
ndege kukodi kutoka kwenye mashirika ya kikanda ya kudhibiti nzige
wekundu na nzige wa jangwani ambazo wakati mwingine hazipatikani wakati
zinazohitajika.
Kufuatia
hali hiyo amesema Wizara katika mwaka wa fedha 2012/13 imekamilisha
viwango vya kiufundi (Technical Specifications) kwa ajili ya kutangaza
zabuni ya ununuzi wa ndege moja ya kunyunyuzia viuatilifu.
---
SERIKALI ITAENDELEA KUWAENDELE ZA WACHIMBAJI WADOGO WADOGO NCHINI
SERIKALI
inatekeleza mkakati wa kuwaendeleza wachimbaji wadogo wadogo wa madini
nchini kwa kuwatambua wao na mahitaji ya mitaji na vifaa ili kutekeleza
kazi yao kwa ufanisi.
Kauli
hiyo imetolew na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Julius
Masele wakati akijibu swali na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini
Stephen Ngonyani leo mjini Dadoma aliyetaka kujua ni lini wachimbaji
wadogo wadogo wa Ng’ombeni, Kalalami, Kigwase watatambuliwa na Serikali
na kupewa kipaumbele kwenye uchimbaji, na kupewa mikopo ya kujikimu
wakati wakitafuta Madini.
Amesema
kuwa katika kutambua umuhimu wa wachimbaji wadogo wadogo Wizara hiyo
imeshakwishatoa imetoa jumla ya viwanja 612 vya uchimbaji mdogo wa
madini katika maeneo ya Ng’ombeni, Kalalani na Kigwase ikiwa ni hekta
3,864.
Aidha,
Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa Serikali kupitia Shirika la Madini la
Taifa na Wakala wa Jiolojia inaendelea kubainisha maeneo yanayofaa kwa
uchimbaji mdogo ili yaweze kutengwa kisheria na kugawiwa kwa wachimbaji
hao.
Masele
alisema kuwa katika utekelezaji wa mkakati huo unashirikisha wachimbaji
wenyewe kwa kuimarisha vyama vyao vya kimkoa na chama cha kitaifa
(FEMATA) na kujadili masuala yao katika vikao vya pamoja vya kila baada
ya miezi sita baina ya wawakilishi wao na Wizara.
Ameongeza
kuwa Wizara ya Nishati na Madini inakamilisha taratibu za Mfuko rasmi
wa kuwaendeleza wachimbaji wadogo ili kuwawezesha kupata mikopo ya vifaa
vya uchimbaji wenye tija.
Aidha
, Naibu Waziri huyo amewasisitiza wachimbaji wadogo wadogo kuwa mikopo
hiyo wanayopata inapaswa itumike vizuri katika malengo waliyoombea ili
wajihakikishie kuzalisha madini mengi na kujiongezea kipato.
--
UDHIBITI WA VISUMBUFU VYA MAZAO
SERIKALI
itafufua kituo cha Kilimo Anga kwa kukiwezesha kuwa na ndege na
Wataalam ili kujenga uwezo wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Masoko
kudhibiti milipuko ya visumbufu vya mazao hasa Nzige.
Hayo
yameelezwa na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi
Christopher Chiza wakati akiwasilisha Bungeni Makadilio ya mapato na
matumizi ya Wizara hiyo leo.
Mhe.
Chiza amesema kwa kiasi kikubwa Serikali imekuwa ikitegemea huduma ya
ndege kutoka kwenye mashirika ya kikanda ya kudhibiti nzige wekundu na
nzige wa jangwani ambazo wakati mwingine hazipatikani wakati
zinazohitajika hali ambayo husababisha Wizara kutegemea kukodisha ndege
kutoka sehemu nyingine.
Amesema
Wizara katika mwaka wa fedha 2012/13 imekamilisha viwango vya kiufundi
(Technical Specifications) kwa ajili ya kutangaza zabuni ya ununuzi wa
ndege moja ya kunyunyuzia viuatilifu.
Aidha,
Wizara itaweka utaratibu wa kuingia ubia na makampuni binafsi na
taasisi zinazotoa huduma kama hizo ili kukijengea uwezo kituo cha Kilimo
Anga.
Wakati
huo huo, Wizara ya Kilimo, Ushirika na Chakula ilisambaza lita ,6000 za
kiuatilifu cha kudhibiti milipuko ya viwavijeshi katika mikoa ya Rukwa,
Katavi, Mbeya, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Geita. Dodoma, Morogoro na
Tanga kunusuru hekta 16,418 za mazao ya nafaka.
---
SERIKALI IMEFANIKIW A KUONGEZA WATAALAM WA KILIMO NCHINI HADI KUFIKIA 7,974
Wataalam
wa ugani wameongezeka kutoka 3,379 waliokuwepo mwaka 2007 hadi kufikia
7,974 mwezi Juni jana(2012) baada ya Serikali kuajiri wahitimu kutoka
vyuo mbalimbali nchini.
Hayo
yamesemwa leo mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na
Ushirika, Mhe. Adam Kighoma Malima wakati akijibu swali Mhe. Mch. Dk.
Getrude Rwakatare (Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi).
Amesema
kuwa mwaka 2007 Serikali ilifanya tathmini ya upatikanaji wa huduma za
ugani nchini na kubaini kwamba mojawapo ya vikwazo vikubwa vya
upatikanaji wa huduma za ugani kwa ufanisi nchini ni upungufu mkubwa wa
wataalam.
Malima
ameongeza kuwa matokeo ya tathmini hiyo yalionyesha kuwa kulikuwepo na
wataalam 3,379 nchini ikilinganishwa na mahitaji halisi ya wataalam
15,082.
Amesema
katika kukabiliana na changamoto hiyo , Serikali ilianza kutekeleza
Mpango wa kuimarisha huduma za Ugani nchini ambapo kuanzia mwaka 2007
Serikali imevifufua vyuo 13 vya kilimo nchini (MATIs) vilivyo chini ya
Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika.
“Ukarabati
mkubwa wa vyuo vitatu MATI Ukiriguru, Maruku na Naliendele-Mtwara na
ukarabati mdogo kwa baadhi ya vyuo kumi vingine umefanyika”. Mhe. Malima
alisema.
Aidha,
Mhe. Malima amesema kuwa vyuo viwili vya mashirika yasiyo ya kiserikali
vilishirikishwa katika kutoa mafunzo yaliyolenga kuongeza idadi ya
wataalam wa Ugani na vyuo hivo kwa sasa vina uwezo wa kudahili wanafunzi
3,500 kwa wakati mmoja ikilinganishwa na uwezo wa kudahili wanafunzi
600 uliokuwepo kabla ya mwaka 2007.
* Habari zote za Bunge na Benedict Liwenga-Maelezo, Dodoma.