Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP Linus Sinzumwa akitoa taarifa ya tukio la kukamata bunduki ya kijeshi SMG kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha). Bunduki hiyo inayodhaniwa kutumika kwenye matukio ya uhalifu, imekamatwa katika kijiji cha Mwamangembe jimbo la Manyoni magharibi.
Afisa upelelezi wa makosa ya jinai (RCO) mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka (wa kwanza kulia) akifuatilia taarifa ya kukamatwa kwa bunduki ya kijeshi aina ya SMG  iliyokuwa ikitolewa na kamanda wa polisi mkoa wa Singida,Linus Sinzumwa.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu
Jeshi la polisi mkoani Singida, limefanikiwa kukamata bunduki ya kijeshi aina ya SMG na risasi zake 28, inayodhaniwa kuwa hutumika katika matukio ya uhalifu.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida Linus Sinzumwa amesema bunduki hiyo wameikamata Aprili saba  saa saba usiku katika kijiji cha Mwamangembe tarafa ya Itigi jimbo la Manyoni magharibi.