Tuesday, April 2, 2013

MBINGA UNITED YAICHAFUA HOLY FAMILY YA SONGEA

Na Fulmence Mbunda ,Songea

LIGI ya Wilaya Mkoa ikiwa inaendelea hatua ya sita bora mkoa wa Ruvuma Timu ya soka Mbinga United ya wilaya ya mbinga imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wapizani wao timu ya soka Holy Family ya Songea mjini mchezo uliochezwa katika uwanja wa Mbinga Mjini.
 
    Katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo  timu zote mbili ziliingia uwanjani zikiwa na nguvu sawa zikijalibu chambuliana lango la mwezake lakini hadi dk 45 ya kipindi hicho timu zote mbili zilitoka uwanja ya bila kufungana .

       Kipindi cha pili dk 70 philipo mawawa aliifungia goli la kwanza katika  timu ya soka mbinga united mpira ambao ulikuwa cheza ni kucheze katika lango la holy family baada ya mabeki wa timu hiyo kushindwa kuokoa mpira huo.
 
     Hadi  muamuzi wa kati Yusufu Ngwaje kutoka wilaya ya  Tunduru  ambaye aliyeongoza mchezo huo alipopuliza kipenga cha mwisho cha mchezo huo mbinga united -1- na holy family hawakupata kitu.
 
   Kwa upande wa kocha wa timu ya holy family Denis John alipozungumza na Demashonews kwa njia ya simu ya kiganja   alisema kuwa wamekubaliana matokeo ijapo mabeki wake wameshindwa kutumia mbinu ya kuokoa goli hilo lakini wanaimani ya kuweza kushinda mechi zingine zilizo baki na kikosi chake kipo vizuri hana wasiwasi kwa mashindano hayo.
 
    Hata hivyo john aliulalamikia uwanja wa michezo wa  mbinga kwa kusema kuwa haujawa mzuri katika kuchezea mashindano yeyote ikiwemo  kiwilaya au mkoa hilo ni nitatizo  ambalo limewapelekea kufungwa kwa timu yake na aliwataka wachezaji wake kukubaliana na matokeo hata pia na uwanja huo.
 
     Katika matokeo hayo timu ya soka Mbinga United imeanza vizuri kwa kuanza kujipatia pointi 3 na goli moja katika ligi hatua ya sita ya wilaya ambopo bingwa wa mashindano hayo hatakuwa ni mchindi wa kanda na kujipatia kitita cha shilingi laki moja.