Tuesday, April 9, 2013

Taswira za Waziri Mkuu Mizengo Pinda Nje ya Viwanja Vya Bunge Mjini Dodoma Leo

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozana na Mbunge wa Iramba magharibi, Mwigulu Lameck Nchemba  kutoka kwenye ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma leo Aprili 9, 2013.
Waziri Mlkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Viti Maalum, Mkiwa Adam Kimwanga kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Aprili 9, 2013.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
--
Wabunge wa bunge la Tanzania leo hii wanakutana mjini Dodoma katika kikao cha bunge mkutano wa  11 mkutano ambao ni mahsusi kwa kujadili bajeti ya serikali.

Akizungumzia kikao hichi Naibu spika wa Bunge la Tanzania Mh. Job Ndugai amesema kwa kawaida katika bunge la miaka mitano huwa linakuwa na mikutano 20 na huu mkutano wa 11 utajadili bajeti ya serikali na matumizi ya rasilimali za nchi namna zitakavyo gawanywa kwa manufaa ya watanzania.

Amesema mkutano huo utafanyika mwezi wote wa nne, wa tano na wa sita.
 
Chanzo hakingowi.blogspot.com