Picha siyo ya tukio
Na Amon Mtega,
Songea.
JESHI la polisi mkoani Ruvuma juzi limelazimika kuwatawanya kwa mabomu madereva pikipiki maarufu kwa jina la
yeboyebo wa manispaa ya Songea mkoani humo baada ya madereva hao kuandamana
kuleekea kituo cha polisi cha mjini hapo kwa lengo la kushinikiza jeshi hilo
liwaachie madereva wenzao wawili walioshikwa na pikipiki zao kufuatia makosa
waliokutwa nayo.
Akiongea na kwa njia ya simu kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimek alisema
kuwa mabomu hayo ya kuwatawanya yalitumika kufuatia vitendo
vya madereva kutaka kuzuia kazi ya polisi katika utendaji wake usifanikiwe.
Tukio hilo lilitokea
April 5 mwaka huu majira ya saa 11.30jioni
katika kituo kikuu cha polisi kilichopo mjini hapo baada ya madereva hao
kuandamana na mapikipiki yao kwa lengo la kushinikiza wenzao wawili walioshikwa
na pikipiki zao kufuatia makosa waliokutwanayo kwenye pikipiki hizo
kinyume na sheria za barabarani na kulitaka jeshi hilo liwaachie.
Nsimek alisema kuwa
kinachofanywa na madereva pikipiki hao hakiwezi kukubalika kwa kuwa ni kinyume
cha sheria cha kulizuia jeshi la polisi linapofanya kazi yake na kuwafanya
wananchi washindwe kupata huduma ya usalama na mali zao kikamilifu.
“Mimi kama kamanda siwezi
kukubaliana na baadhi ya vitendo vinavyofanywa na madereva pikipiki hao kwa
kutaka wao waonekane wapo juu ya sheria jambo ambalo haliwezekani kabisa ni
lazima kila mmoja atii sheria bila suluti”alisema kamanda huyo.
“Naomba madereva
pikipiki wanielewe kwamba ni lazima sheria zifuatwe na siyo mambo wanayoyataka
ya kushindana na jeshi la polisi bila sababu za msingi na kuwafanya wananchi
waishi katika hali ya hofu”alisema Kamanda Nsimeki.
Aidha kamanda huyo hakuweza kuwataja majina ya
madereva pikipiki waliokamatwa kwa makosa yaliyodaiwa kuwa ni uzembe barabarani
kwa kuwa jeshi hilo
linaendelea kulifanyia kazi.
Kwa upande wao wananchi waliokuwa wakitimua mbio kufuaatia
mabomu hayo ambao majina yao
hayakutambulika walisikika wakisema kuwa
sasa serikali inatakiwa iangalie upya namna ya utoaji elimu kwa madereva
pikipiki hao pamoja na kuzitambua sheria ili kuepusha malumbano ambayo
yameshaanza kuota sugu.