Kaimu katibu tawala mkoa wa Ruvuma ndugu Severine Tossi kushoto akiwa na Mratibu wa kanda nyanda za juu kusini Bi Atuganile Jonas
katika unguzi wa uhamasishaji wa ajira katika sekta ya afya nchini kwa wanafunzi wa vyuo vya afya mkoani Ruvuma.
Katibu wa Afya manispaa ya Songea mjini Bw. George Mhina akifatilia kwa makini washa ya uhamasishaji wa ajira katika sekta ya afya nchini kwa wanafunzi wa vyuo vya afya mkoani Ruvuma
.................................................
.................................................
Taasisi hii ya Benjamini William
mkapa HIV/AIDS imeendela kwa kuandaa
maonyesho ya uhamasishaji wa ajira katika sekta ya afya nchini kwa wanafunzi
na wahitimu wa vyuo vya afya katika manispaa ya songea.
Kwa hivi sasa sekta ya
afya inakabiliwa na upungufu wa wataalam wa afya sehemu zote nchini lakini hali
hii imeathiri zaidi sehemu za vijijini ambako ndiko waliko watanzania wengi.Kutokana
na hali hiyo serikali nayo imeweza kujipanga ikishirikiana na wadau mbalimbali ili kuweza kuinusuru hali ngumu ya
kutokuwa na wataalamu wa kutosha.
Mikakati na miongozo
mbalimbali inatekelezwa ikiwemo mpango Mkakati wa tatu wa Sekta ya Afya(Health
Sector Sector Strategic Plan).Mipango iliyoainishwa kwenye mikakati hii ni pamoja na kuweza
kuhakikisha kuwa wanapatikana wataalamu
wa kutosha ili waweze kuajiriwa na kutoa
huduma zenye ubora kwa wananchi walio wengi. Hii ni pamoja na kuahamasisha
wataalam wanaohitimu katika vyuo vya mafunzo waweze kuajiriwa katika sekta ya
afya ili kuweza kuongeza idadi ya wataalamu wanaotoa huduma.
Katika
hutuba iliyotolewa na Kaimu katibu tawala mkoa wa Ruvuma ndugu Severine Tossi katika chuo cha maafisa
tabibu songea amesema malengo ya uhamasishaji huu ni kuelimisha juu ya nafasi
za ajira katika halmashauri za wilaya
katika mkoa wa Ruvuma , Maboresho yaliyofanyika katika sekta ya afya na maslahi
ya mfumo wa utunzaji, upatikanaji na ubadilishaji wa taarifa za wahitimu kati
ya vyuo na waajiri (wizara husika na Halmashauri).
“ Ninaomba niwaase
wanavyuo kuwa serikali inajitahidi kuboresha maslahi ya watumishi wake wote
pamoja na wa sekta ya afya, Sisi ni mashuhuda
na tumeona ni jinsi gani basi
ajira katika sekta ya afya imeongezeka
mwaka hadi mwaka, pia imeendelea kutambua kada ambazo hapo awali
hazikuwepo . Hii ni ishara kuwa serikali inajali na hivyo mna kila sababu za
kukata shauri la kujiunga na sekta ya
afya”
Nae Atuganile Jonas ambaye ni Mratibu wa kanda nyanda za juu kusini
amesema mbali na zoezi la uhamasishaji wa ajira katika halmashauri za mikoa
mbalimbali hapa nchini Tanzania pia wameajili wa tumishi wa afya amabo wamepelekwa
kwenye halmashauri mbalimabali “watumishi hao wapo chini ya taasisi kwa mkataba
maalumu baada ya hapo halmashauri husika uwauwisha katika ajira ya serikali na
kuwa watumishi wa umma”
Atuganile
ameongezea kwa kusema taasisi hii ya Benjamini William mkapa HIV/AIDS
Foundation inamradi wa ujenzi wa nyumba katika halmashauri sabani katika mradi huo halimashauri moja hujengewa
nyumba kumi mpaka sasa mkoani mtwara na lindi tayali wameshakamilisha na
kukabidhi nyumba hizo.
Na kwa mkoa wa Rukwa na Katavi nyumba zimeshakamlika bado
makabidhiano na kwa upandea wa mkoa wa Ruvuma halmashsuri nne zitajengewa nyumba
kumi kwa kila halmashaur moja ,nakati ya halmashauri hizo ni mbinga , namtumbo.
Tunduru,songea vijijin,
Vilevile taasisi ya
Benjamini William mkapa HIV/AIDS Wanaufadhiri
wa wanafunzi ambao wanaoenda kusoma katika vyuo vya afya kwa wale ambao wamefauru
kwa kiwango lakini hawana uwezo kutokana na hali zao za kimaisha , Hadi sasa
wanafunzi 150 wapo vyuooni kutokana na taasisi hii imeingia mkataba na
halmasharu pamoja na wanafunzi kwa kuwapa msaada wa kuwaghalamikia masomo na
baada ya kumaliza masomo yao watarudi katika halmashauri zao na kufanya kazi .