MFANYABIASHARA,
Mkumbukwa John Shayo (37) (pichani) aliyefariki katika kifo chenye
utata nchini China amezikwa Jumatano iliyopita na kulifanya Jiji la
Mwanza kutawaliwa na majonzi.
Baadhi ya waombolezaji wakitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lililobeba mwili wa marehemu Mkumbukwa Joseph.
Umati wa
watu ulihudhuria mazishi hayo nyumbani kwa bibi wa marehemu, Mabatini
kisha kuelekea katika Makaburi ya Buzuruga, Nyakato na kila mtu
alionekana kujawa na huzuni.
Hata hivyo, mazishi hayo yaliathiriwa
kidogo na mvua iliyofanya baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki washindwe
kuuaga mwili wa marehemu.
Watu wakipita kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Josephat Mkumbukwa. Kushoto ni mjomba wa marehemu Erasto Kombe.
Mkumbukwa
alifariki China na maiti yake kuhifadhiwa hospitali kwa takriban mwaka
mzima na serikali ya nchi hiyo huku mkewe, Neema Majukano pamoja na
rafiki wa marehemu aitwaye Haji Msongore wakilaumiwa kwa kushindwa kutoa
taarifa mapema juu ya kifo hicho.
Paroko
wa Kanisa Katoliki Kigango cha Mabatini Nyamagana, Charles Bundu,
akiendesha ibada ya kuuombea mwili wa marehemu Joseph Mkumbukwa aliyeuwa
nchini China mwaka jana.
Aidha,
utata umegubika kifo cha Mkumbukwa kufuatia rafiki huyo wa marehemu
ambaye mara ya mwisho walikwenda wote nchini Chini kudaiwa kumuoa mke wa
marehemu, Neema.
Dada wa marehemu akisaidiwa na waombolezaji mara baada ya kuuaga mwili wa marehemu kaka yake
Hata hivyo, mazishi hayo yaliathiriwa kidogo na mvua iliyofanya baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki washindwe kuuaga mwili wa marehemu.