Na Nathan Mtega,Songea.
JUMLA ya watoto 250 wa Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wanaoishi katika mazingira hatarishi jana wamepata
kadi za mfuko wa afya kwa jamii [CHF]zitakazofanya watibiwe bure kwa muda wa
mwaka mmoja .
Watoto hao
wamekabidhiwa kadi hizo kupitia shirika lisilo la kiserikali la ROA linalo
fanyakazi ya kuwahudumia watu waishio katika mazingira hatarishi ikiwemo na
wagonjwa waliopo majumbani mkoani hapo.
Awali Mwenyekiti wa
shirika hilo Mathew Ngalimanayo akitoa taarifa
mbele ya mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti ambaye alikuwa mgeni rasmi
ka zoezi hilo la ugawaji wa kadi hizo kwa watoto
hao alisema kuwa shirika hilo
linafanya kazi ya kuwahudumia watu waishio katika mazingira hatarishi na
wagonjwa majumbani.
Ngalimanayo alisema
kuwa shirika hilo
mpaka sasa limeweza kusaidia watoto 613 waishio katika mazingira hatarishi na
kuwa pia wanafanya kazi ya kuwapima afya kwa baadhi ya watu wanaohitaji kujua
mwenendo wa afya zao hasa katika ugonjwa hatari ya ukimwi.
Kwa upande wake
mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti akipokea taarifa hiyo alisema kuwa
shirika hilo
limeonyesha njia namna ya uhudumiaji wananchi waishio katika mazingira
hatarishi tofauti na baadhi ya taasisi ambazo kazi yake zikipata fedha kwa
wafadhili ni kula.
Mkirikiti alisema
kuwa taasisi za mtindo huo ni lazima azifute kwenye wilaya yake kwa kuwa
hazifanyi kazi ambayo ilitarajiwa na wafadhili wanaowapatia misaada mbalimbali
ikiwemo ya fedha.
Alisema kuwa hatanii atazifungia hizo taasisi
kwa kuwa zinajinufaisha kupitia migongoni mwa watu waishio katika mazingira
hatarishi kwa kutowasaidia kama maeelekezo ya maombi yao kwa wafadhili waliowapatia misaada.
Alisema kuwa hajapata kuona taasisi inayohudumia na kufuata
taratibu zilizowekwa na wafadhili kama shirika hilo la ROA na kutaka asasi nyingine zisizo
za kiserikali kuiga mfano wa shirika
hilo.alima mkuu huyo wa wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti.
Mwisho.