Sunday, April 7, 2013

Kisomo cha Kumuombea Dua Marehemu Mzee Abeid Amani Karume Zanzibar

 

Wananchi na Waumini wa Dini ya Kiislamu wakisoma Hitma Kumuombea Dua Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,katika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya CCm Kisiwandui Mjini Zanzibar,ambapo kila ikifika siku kama hii wananchi kwa ujumla wao hukusanyika kuomba dua kama hii.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaj Dk.Jakaya Mrisho Kikwete,akisalimiana na wakuu wa Vikosi vya ulinzi alipowasili katika viwanja vya Ofisi ya CCM Kisdiwandui Mjini Unguja kuhudhuria katika Hitma ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.

Wake wa Viongozi Wakuu wakiwemo na viongozi wa taasisi za Kinamama wakinyanyua mikono juu kumuombea dua Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.katika kaburi lake huko CCM Kisiwandui mjini Zanzibar,baada ya kisomo cha Hitma leo

/Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na wakuu wa Vikosi vya ulinzi alipowasili katika viwanja vya Ofisi ya CCM Kisdiwandui Mjini Unguja kuhudhuria katika Hitma ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume

Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume,(kulia) akiwa na Wake wa Viongozi mbali mbali katika Hitma ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,huko Ukumbi wa CCK Kisiwandui Mjini Zanzibar Leo.

Akina mama wa Kiislamu wa Mjini Magharibi Unguja wakijumuika na Viongozi wengine katika kisomo cha HItmaya Kumuombea Dua Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar