Na
Steven Augustino, Tunduru
WAKATI Chama
cha Mapinduzi (CCM) kikidai kujipanga kuunganisha na kuimarisha nguvu kwa
viongozi wake nchini Wilayani Tunduru Mkoni Ruvuma hali imekuwa ni tofauti
baada ya viongozi wa chama hicho kuanzisha mgogoro wa kugombania kubadilishana
cheo.
Hayo
yamebainika kufuatia kuwepo kwa mvutano huo wa chini kwa chini kushindwa
kupatiwa dawa na uongozi wa CCM Mkoa na Wilaya juu ya madai ya Mjumbe wa
Mkutano Mkuu wa CCM Taifa (Mneki) Alhaji Ajili kalolo kutaka kubadilishana Cheo
chake hicho na Mweyenkiti wa Ccm Wilaya ya Tunduru Bw.Hamisi Kaesa.
Kufuatia
hali hiyo hivi sasa Mwenyekiti wa CCM Wilaya amedaiwa kuwa amekuwa akilazimika
kuvunja itifaki hiyo na maelekezo ya Chama na kumpisha mneki huyo akae kiti cha
mbele ili aweze kujiridhi katika roho yake.
Taarifa za
malumbano hayo yaliyosababisha kuzuka kwa mgogoro huo pamoja na matukio ya
vitisho vya maneno makali na vijembe miongoni mwa viongozi hao yanadaiwa
kuanzisha na Alhaji kalolo ambaye inadaiwa kuwa anahitaji kutukuzwa na kupishwa
akae mbele kwa lengo la heshima ya kuonekana kuwa yeye ndiye anayepeperusha
Bendera ya Chama hicho kaatika misafara yote.
Suala hilo
ambalo limezua utata na kusababisha mtafaluku mkubwa kati ya viongozi hao
linadaiwa kuwa chanzo chake ni Mneki huyo kutoridhishwa na kukubaliana na
maelekezo ya itifaki za chama chake zinazoelekeza kuwa Viongozi wote wenye
nafasi na cheo kama chake inawataka kukaa kiti cha nyuma cha gari inapotokea
yeye na mwenyekiti huyo wanasafiri kwa pamoja.
Aidha
taarifa hizo zilizo dhibitishwa na viongozi wa CCM Wilaya ya Tunduru na Mkoa wa
Ruvuma ambao waliomba wasitajwe majina yao gazetini zinaeleza kuwa Bw. Kalolo
ambaye mahitaji yake wakati wa kuingia katika mchakato huo yalikuwa ni kutafuta heshima na kutukuzwa
hivi sasa anajutia na kuulaumu uongozi uliopita katika chama hicho kuwa
walimuuza kutokana na kumshawishi agombee nafasi hiyo ambayo inaonesha
kutokidhi haja za malengo yake.
Alipotakiwa
kuzungumazia mgogoro huo Mweenyekiti wa CCM Wialaya ya Tunduru Bw. Hamisi Kaesa
alisema kuwa tatizo hilo kwa sasa ni kubwa na haelewi jinsi ya kuliepuka
kutokana nay eye kutokuwa na mamlaka ya kubadilishana nafasi hizo zaidi ya
maamuzi ya kura zilizopigwa na wajumbe wa mkutano mkuu ulio wachagua.
“tatizo hili ni kubwa na hivi sasa kuna
mgogoro mkubwa kati yangu na Mneki, lakini hivi sasa mimi nimekuwa
nikijishuhsha na kumpisha yeye akae kiti cha mnbele ili aweze kujiidhisha nafsi
yake ingawaje mimi na viongopzi wa chama Wilayani tumekuwa tuki kiuka miongozo
na itifaki ya Chama” alisema Kaesa.
Juhudi za kumtafuta Mjumbe huyo wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa (Neki) alihaji Ajili
Kalolo ili aweze kujibu tuhuma hizo hazikuzaa matunda kutokana na kutopatikana katika simu yake
Mwisho