Kaimu mkuu wa mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Mkuu wa wilaya Mh.Joseph Joseph Mkirikiti akisisitiza jamba kwa wanakijiji wa Palangu alipo tembele shamba la mkulima Bw. Isaya Mwilamba
Mmilikiwa Shamba Bw. Isaya Mwilamba akimwelekeza siri ya mafanikio yake ya kujiwekeza katika kilimo chake kaimu mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mh.Joseph Joseph Mkirikiti
Kaimu mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mh. Joseph Joseph Mkirikiti akionyeshwa jinsi mhindi beba punje za mahindi vizuri katika shamba la muwekezaji
Shamba la muwekezaji lenye ukubwa hekali 250
Mmiliki wa Blog ya demashonews toka kulia akiwa na mwandishi wa habari
wa Star TV Adamu Nindi nao walikuwepo katika kuchukua habari
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Ruvuma akiwa ameongozana na wadau mbalimbali pamoja na mmiliki wa Shamba akikagua shamba
Hii ndio Hotel anayo miliki kutokana na uwekezaji wa kilimo
..............................................................................
Kaimu mkuu wa mkoa wa ruvuma ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya
songea Joseph Joseph Mkirikiti amefurahishwa na mkulima wa
mjini humo Bw .
Isaya Mwilamba ambaye amepata
mafanikio makubwa kupitia kilimo cha kisasa na kuwataka wakulima wengine
kumuiga mkulima huyo.
Alionyesha kufurahishwa na mkulima huyo baada ya kutembea shamba
la mkulima huyo lenya ukumbwa zaidi ya hekali 250 ambalo limestawi vizuri kutokana
na kulima kwa kufuata kanununi bora za kilimo na kuzingatia matumizi ya mbegu
bora.
Kaimu Mkuu wa mkoa huyo akizungumza katika kijiji cha
palangu songea vijijini ambako mkulima huyo amelimia shamba hilo alisema mambo
mazuri haya fanywi na wazungu pekee kwani mkulima huyo ameonyesha wa tanzania wanaweza kufanya mambo
makubwa
“ Jamani wenyewe
simumeona hili shamba limelimwa na wazungu?
Ni kweli wakulima wengine mnapaswa kumuiga Mwilamba ambaye amepata mafanikio makubwa kupitia kilimo na kujenga
hotel ya kisasa yenye thamani ya kuzidi
bilioni moja “
Kwa upande wake mmoja wa wakulima wakubwa wa mkoa wa ruvuma Bw. Isaya Mwilamba ameiomba serikali
kuanzisha Bank ya wakulima na kubainisha kwamba
bank hiyo itakuwa ni mkombozi kwa wakulima kwa kuwa itakuwa ikitoa mkopo
kwa mashariti nafuu kuliko bank zilizopo sasa
ambazo zinamuona mkulima ni mtu asiekopeshaka .
Mkulima huyo amefafanua kuwa bank zilizopo sasa zimekuwa
zikimtaka mkulima aonyeshe hati ya nyumba
pindi anapotaka kukopa kwenye bank hizo wakati wakulima waliowengi
hawana hati za nyumba na pia hawana
nyumba bora ambazo zinaweza kuwa dhamana ya mkopo.