MABONDIA wa ngumu wa wilaya ya Songea mkoani Ruvuma wameanda pambano la ngumi agosti 8 mwaka huu
ilikuwata wapenzi na wadau wa mchezo huo wawaeze kutoa hudhamini wa michezo
hiyo,ambao utafanyika kwenye uwanja wa maji maji songea mjini.
Mmoja wa washiriki mkuu wa mchezo huo Mussa Omary alisema kuwa
pambano hilo
wameanda wakiwa na lengo kubwa la kutafuta hudhamini katika michezo ya ngumi
kwa kuwa wadau wengi wameusau mchezo huo jambo ambalo wanashindwa hata kwenda
kushiriki mashindano mbalimbili ya mchezo huo.
Alisema kuwa
pambano hilo litakuwa ni moja ya kuwapatanisha baadhi ya wanamichezo wa ngumi
na kuwataka kuwa wabunifu wa kuweza kujishirikisha na mambo mbalimbali ikiwa ni
moja ya kuendeleza ngumi katika mkoani humo na kwa kuwa maporomota wengi kuwa
feki ambapo jambo lingine linalo wachangia kukosa kwa wadhamini.
“tumeanda pambano
sisi wenyewe ambalo litakuwa nzuri na lengo kubwa la kuandaa pambano hilo
kwanza kuwataka wanadau na wapenzi wa ngumi waweze kutuchangia ,pili ikiwa ni
moja ya kuwakutanisha mabondia wa ngumi hasa mkoani hapa kwa kuwa mabondia
wamekuwa maporomota feki wanaweza kuandaa pambano lakini wanashindwa kufuata
utaratibu hivyo pambano hilo litakuwa la kuwalekebisha baadhi ya
mabondia.”alisema Omary
Hata hivyo Omary
alimtaja bigwa ambaye atapigana naye siku ya pambano hilo kuwa ni Oborti Ameme
wa kutoka Mbeya ambapo alisema kuwa yeye anashikiria mkanda wa Taifa kwa kuwa
na kilo 59 na huyo bondia toka Mbeya hanarekodi yeyote na Saimoni Mwakwenda atapigana na Maisha Samsoni wa kutoka Mbeya.
Omary aliwataja
mabondia wengine ambao watashiriki mchezo huo kuwa ni Alibabu wa songea na
Kenedi Kitenge wa kutoka Iringa,Sunusa
Bakari wa songea na Taisoni wa kutoka Mbinga na Jemusi Mtanga wa Songea na
Furaha Tengeni wa kutoka wilaya ya kyera.
Hata hivyo omary
aliwataka wadau na wapenzi hasa wakiwemo viongozi wa mkoani hapa kutoa hudhami wa michango mbalimbali ili
kuweza kukuza na kuendeleza mchezo wa
ngumi ikiwa mchezo huo ni mchezo hunao pendwa na watu wengi katika sehemu
mbalimbali.