Sunday, April 21, 2013

VIKWAZO VINAVYOCHANGIA KUSHUKA KWA ELIMU WILAYA YA TUNDURU MKONI RUVUMA HIVI NI MOJA WAPO

  picha sio ya tukio halisi
Na Steven Augustino, Tunduru
 Imebainishwa kuwa Mahusiano mabaya kati ya Walimu na Wanafunzi na
 Wanafunzi wadaiwa kukataa kukaa katika mabweni na Hosteli ni miongoni
 mwa vikwazo vya maendeleo ya elimu Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma na
 kupelekea Wilaya hiyo kupata matokeo mabaya kwa wanafunzi waliofanya
 mitihani ya Kidato cha pili na cha nne katika kipindi cha mwaka 2011/2012 .

 Hayo yalibainishwa na afisa elimu Sekondari Mwl. Ally Mtamila wakati
 akiwasilisha taarifa ya matokeo ya kidato cha pili na cha Nne
 katikakipindi cha mwaka 2011/2012,

  Kwa mujibu wa tarifa hiyo mwaka 2011 matokeo ya Kidato cha pili Wilaya
 hiyo ilifaulisha kwa wastani wa asilimia 35%, huku takwimu hizo kwa
 upande wa matokeo ya Kidato cha Nne katika kipindi cha mwaka 2012
 zikionesha kuwa Wilaya hiyo ilifaulisha kwa wastani wa asilimia 59.46%
 kiwango kilichodaiwa kuwa ni kidogo na kiliifanya Wilaya yao kushika
 nafasi ya mwisho kimkoa.

 Awali aikifungua Mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Tunduru  Chande Nalicho
 pamoja na kubainisha kuwa pamoja na serikali kuwa na vipaumbele
 vingine vya maendeleo lakini Elimu ni muhimu ilikujiletea mabadiliko
 ya kweli.

 Dc nalicho aliendelea kueleza kuwa Ili kuwaletea maendeleo wananchi wa
 Tunduru ni lazima wilaya ijikite katika kusimamia elimu na kuhalalisha
 uwepo wao na kwamba wasipo wakazania kusomaa shule maendeleo
 yanayopiganiwa na serikali hayatakuwa na maana yoyote kwao.

 Katika taarifa hiyo Mkuu Dc. Nalicho akatolea mfano wa Takwimu za
 ufaulu wa wanafunzi 2764 waliochaguliwa kujiunga na masomo ya
 sekondari  hadi mwishoni mwa mwezi wa tatu ni asilimia 60% ya  watoto
 wote waliochaguliwa  kujiunga na masomo ya sekondari.

  Akizungumzia upande wa Shule za Msingi  Mwaka 2011Shule ya Msingi
 Nakapanya ilifaulisha Watoto 26 lakini takwimu zinaonesha kuwa  watoto
 wote hawakwenda shule na kuongeza kuwa hali hiyo inawakatisha tama
 hata walimu wa shule za msingi zinazofaulisha watoto hao .

 Wakichangia kwa nyakati tofauti Mwl. Issa Ngajime alisema kuwa chanzo
 cha kushamiri kwa utoro,uchangiaji hafifu wa chakula mashuleni na
 wanafunzi kukataa kukaa katika hostel zilizojengwa katika shule zao
 Viongozi wa serikali za Vijiji wanasitahili kubeba lawama huku
 wakiwataka viongozi kutochanganya elimu na Siasa kwa kuboresha mbinu
 za kufundishia na kuchukua hatua kwa Wanafunzi ambao wamekuwa
 wakibainika kuchaguliwa wakiwa hawajui kusoma,kuandika na kuhesabu.

  Mkuu wa shule ya Mgomba Mwl. Elis Banda alisema kuwa tatizo wanafunzi
 kukataa kukaa katika Hosteli linatokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya
 watoto wanaosoma katika shule hizo kuwa ni wakazi wa maeneo husika na
 akapendekekeza kuwepo kwa utaratibu wa kutenga Shule za kanda kwa
 ajili ya kupeleka wanafunzi kutoka maeeneo tofauti huku akiitaka
 serikali kutoa maelekezo ya vitabu vya kununuliwa tofauti na sasa
 ambapo kumekuwa na maelekezo ya kuwataka wakuu wa shule kutumia vitabu
 kutoka katika kampuni ya EMACK  ambapo alishauri kupunguzwa kwa idadi
 ya vitabu vya kufundishia.

 Wadau hao waliendelea kubainisha vikwazo vingine kuwa ni paomja
 Na wanafunzi kubeba mimba wakiwa shuleni.
Mkuu wa Shule ya sekondari Lukumbule Mwl. Mathias Katto akabainisha
 vikwazo vingine kuwa shule zao kutokuwa na walimu wa masomo ya
 Sayansi,Shule kutokuwa na maktaba,Watoto kutoka katika maeneo husika
 na miundombinu ya Nyumba wanazo ishi nimbovu ,mila na destuli potofu
 za kuwafundisha watoto wadogo hasa wakike mafunzo ya kuishi kiunyumba
 ambayo hutolewa kupitia mafunzo ambayo hutolewa katika jando, Unyago
 na Msondo na ngoma ya Sakamimba hali ambayo imekuwa ikipelekea baadhi
 ya wanafunzi kuishi kwa wanaume huku wakiwa wanaendelea na masomo.