Mhariri
wa Tujifunze, Bw. Christian Sikapundwa (wa kwanza kulia)akiwa katika
picha ya pamoja na Uongozi wa Chuo Kikuu cha St Agustino (SAUT) tawi la
Songea mbele ya Jengo la Utawala. Wengine toka kushoto ni Mhadhiri
Bahati Chale, Dean of Student Michael Sinyenga, Dr. Jeremiah Haraka na
Ofisa Habari na Mawasiliano wa Chuo hicho Stella Ndunguru.Na Juma Nyumayo, Songea.
CHUO Kikuu cha St. Agustino SAUT, tawi
la Songea lenye wanafunzi wapatao 629 kimejipanga vyema kutoa taaluma,
na kusimamia maadili mema ili kuleta ufanisi katika kuendesha shughuli
za elimu chuoni hapo.
Akizungumza leo kwa njia ya Simu na
Blogu hii, Dean of Student, Michael Sinyenga, alisema Uongozi wa Chuo
hicho Unatilia mkazo mambo ya maadili na hivyo wamekwisha waelekeza
wanachuo na wafanyakazi wao namna wanavyotarajia kuhusu mavazi, na
mwenendo mzima wa wanafunzi wawapo Chuoni na nje ya chuo .
"Tutawaangalia hasa kwenye mavazi na matendo yao Chuoni na nje
ya Chuo," alisema Sinyenga. Hivi sasa Manispaa ya Songea na Vitongoji
vyake vimechangamka kibiashara na inategemewa mabadiliko makubwa
yatakuja kwa mahitaji mbalimbali wakati Chuo hicho kitakapodahili
wanafunzi wengi zaidi. Mahitaji hayo ni pamoja na nyumba za kupangisha
wanafunzi na watumishi wa Chuo, wawekezaji na wafanyabiashara
watakaohamia kufuata soko la Idadi ya watu wanaoongezeka katika mji wa
Songea uliopo kusini mwa Tanzania mpakani na nchi ya Msumbiji.
Chanzo ruvumapressblog