Mkuu
wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akitoa hotuba
yake kabla ya kuzindua mabasi mawili na gari ndogo moja (pick-up) kwa
ajili ya kuwasafirishia mahabusu toka gerezani kwenda mahakamani na
kurudi gerezani kwa Mkoa wa Dodoma. Katika hotuba yake mkuu wa jeshi
hilo aliwataka maofisa magereza wa mkoa huo wawe makini kuyatunza magari
hayo. Uzinduzi huo ulifanyika katika Gereza Kuu Dodoma. Picha na
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu
wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (kulia),
akikata utepe kuzindua rasmi jukumu la kuwasafirisha Mahabusu kutoka
Gerezani kwenda Mahakamani na kurudi Gerezani kwa Mkoa wa Dodoma.
Katikati ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mary
Shangali, kushoto ni Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), Dk.Eliezer
Feleshi ambao walikuwa katika uzinduzi huo uliofanyika katika Gereza Kuu
Isanga Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali-Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu
wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja, akiwasha
moja ya magari yaliyozinduliwa kuashiria uzinduzi wa kuwasafirishia
Mahabusu kutoka Gerezani kwenda Mahakamani na kurudi Gerezani kwa Mkoa
wa Dodoma. Uzinduzi huo ulifanyika katika Gereza Kuu Isanga Dodoma.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali-Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Mkuu
wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (kushoto)
akisalimiana na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mary
Shangali baada ya uzinduzi wa mabasi mawili na gari ndogo moja
(pick-up). Kushoto Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), Dk.Eliezer
Feleshi. Uzinduzi huo ulifanyika katika Gereza Kuu Dodoma. Picha na
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Magari
matatu ya kuwasafirisha Mahabusu yaliyozinduliwa na Mkuu wa Jeshi la
Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja, katika hafla iliyofanyika
Gereza Kuu Isanga Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya
Serikali-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.