Monday, April 8, 2013

WABUNGE WAMIMINIKA DODOMA TAYARI KWA KIKAO KE

Bunge la Tanzania linatarajia kuanza Kikao chake kesho jumanne tarehe 09.04.2013 mjini dodoma.Bunge linaanza Kikao chake hicho kesho baada ya wabunge hao kumaliza vikao vya kamati mbalimbali za bunge Jijini Dar es salaam vilivyoanza takribani wiki mbili zilizopita.Wabunge hao kabla ya kuanza vikao hivyo walianza kuchagua Mwenyeviti wa kamati mbalimbali za bunge na kisha kuanza vikao vya kamati pamoja na kutembelea na kukagua shuguli mbalimbali zilizo katika kamati husikia.
IMG_1480
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda Ambaye ni Kiongozi wa Shuguli za Serikali Bungeni akiongozana  na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rehema Nchimbi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Leo Aprili 8,2013 Tayari kuhudhuria kikao cha Bunge kinachotarajiwa kuanza Kesho Aprili 9 Mjini Dodoma
Mkoani Morogoro Eneo la Stendi ya mabasi mikoani msamvu ambapo ni njia panda ya Barabara za mikoa mbalimbali kuwekuwa na msururu wa magari ya  Wahishimiwa wabunge,Mawaziri na manaibu mawaziri pamoja na viongozi waandamizi wa bunge Wakiwa njiani kuelekea Mkoani Dodoma Tayari Kuudhuria Kikao hicho kinachoanza kesho.