Na Nathan Mtega,Songea
WATU wawili
wamefariki dunia na mmoja akijeruhiwa katika
ajali ya gari iliyotokea Aprili 21 mwaka huu majira ya saa 11 jioni katika eneo
la Wino wilayani Songea mkoani Ruvuma katika
bara bara ya Songea-Njombe.
Ajali hiyo
iliyohusisha gari aina ya Scania yenye namba za usajili T 974 ANN iliyokuwa
ikiendeshwa na dereva Festo Elia Kimata(29)
ilipata ajali hiyo katika eneo la Wino mtelemkoni kwa kile kilichoelezwa kuwa dereva
wa gari hilo
alishindwa kuimudu kona hiyo hali iliyosababisha gari kupinduka na yeye kufariki dunia papo hapo.
Mtu mwingine
aliyefariki dunia katika ajali hiyo ni Fausta Mlelwa(35) mkazi wa kijiji cha
Kifagulo kilichopo katika eneo la Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma huku
utingo wa gari hilo
Lufinus Mayemba(32) akijeruhiwa vibaya na kulazimika kukimbizwa katika
hospitali ya Misheni ya Peramiho kwa ajili ya matibabu.
Ajali hiyo imetokea
saa chache baada ya ajali nyingine iliyotokea katika eneo hilo
iliyohusisha gari aina ya NOAH iliyokuwa ikitokea mjini Songea kuelekea jijini
Mbeya ambayo ilisababisha watu kunusurika kifo kwa kujeruhiwa nba kulazwa
katika hospitasli ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma
kwa matibabu.
Kufuatia kuwepo kwa
ajali za mara kwa mara katika eneo hilo baadhi ya wananchi wameiomba wakala wa bara bara(TANROAD) mkoa wa Ruvuma
kuboresha alama za bara barani katika eneoi hilo na pia serikali kuona
uwezekano wa kukiboresha zaidi kituo cha afya cha afya cha Madaba eneo ambalo
limekuwa na ajali nyingi.
Kamanda wa polisi wa
mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki akitihibitisha kutokea kwa ajali hiyo kwa njia ya simu alisema
anawasiliana na mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu ili kuona uwezekano wa
kufanyia lazi maombi ya wananchi hao.
Mwisho.