Mahmoud
Ahmad Arusha
Jeshi la
Polisi mkoani hapa limefanikiwa kuuvunja mpango wauhalifu uliokuwa umeandaliwa
na mtandao wa uhalifu wa mikoa ya Dar es salaam na Arusha wakishirikiana na
walinzi wa kampuni ya ulinzi ya Victoria Support Service katika lindo mmoja la
ulinzi la kampuni hiyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake Kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa
Ibrahimu Kilongo alisema mnamo tarehe 5-3-2013 walipata taarifa kuwa kuna mpango
wa kula njama na kuiba kwenye lindo mmoja la kampuni hiyo ya ulinzi kiasi
kikubwa cha fedha ndipo walianza kufuatilia na kubaini njama
hizo.
Kilongo
alisema kuwa walifanikiwa kuzima jaribio hilo na kuwakamata watuhumiwa kadha
kutoka kwenye mtandao huo wa uhalifu wanaofanya kwenye mikoa ya Dar es salaam na
Arusha na walikiri kutaka kuiba wakishirikiana na walinzi wa kampuni hiyo kwenye
lindo mojawapo la kampuni hiyo.
Akiwataja
watuhumiwa wa mtandao huo kaimu kamanda kuwa ni Hamad Hassan46 mkazi wa
Sanawari,Makanga Ichami 49 mkazi wa Mwanama,Isack Luhanga40 mkazi wa
Ngulelo,Johnson Benjamin35 mkazi wa Moshono,na Samwel Daniel28 mkazi wa Daraja
mbili huku wakiwataja wenzao wa kutoka Dar es salaam.
Kilongo
alisema kuwa huko Usa river kwenye kizuizi cha polisi walifanikiwa kuikamata
gari Toyota Carina rangi nyeupe lenye no. za usajili T 734 BSR iliyobeba
watuhumiwa kutoka Dar na kuwataja kuwa ni Oscar Mziray47,Samwel Mabiba41,Joseph
Zozi22,Ibrahim Kingu49 na Raphael Wiliam28 wote wakazi wa jijini Dar es
salaam.
Watuhumia
hao pia walikamatwa na mitungi mine ya Gas,Mkasi mmoja mkubwa wa kukatia vitu
vizito mitambo miwili ya kuvunjia , pipe moja ya kuunga kwenye mtungi wa
Gasi,mabegi manne na mfuko mmoja wa sulphate iliyokuwa itumike kubebea mitungi
ya gasi na katika mahojiano walikiri kuja Arusha kufanya uhalifu
huo.
Kilongo
alisema upelelezi wa tukio hilo bado uanaendelea na kuwa mara baada ya upelelezi
wa awali kukamilika watawafikishi mahakamani kwenda kujibu tuhuma
hizo.