Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akikabidhi msaada wa shilingi mil. 5 kwa Katibu Mkuu wa Baraza la
Misikiti Tanzania (BAMITA),Sheikh Salum Sung’he kwa ajili ya kuendeleza
mipango kazi wa BAMITA katika kutoa Elimu kwa Jamii juu ya kupunguza
maambukizi ya Ukimwi na Kudhibiti Mimba kabla ya Ndoa.Makabidhiano hayo
yamefanyika leo jijini Dar es Salaam.Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa
Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA),Alhaj Juma Swalehe.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo picha) wakati wa kukabidhi
msaada wa sh. mil 5 kwa Viongozi wa Baraza la Misikiti Tanzana,katika
makabidhiano yaliyofanyika leo Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwa
katika mazungumzo na Viongozi wa Baraza la Misikiti Tanzania
(BAMITA),Alhaj Juma Swalehe (kushoto) na Sheikh Salum Sung’he waliofika
ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam kupokea msaada wa shilingi mil. 5
kwa ajili ya kuendeleza mipango kazi wa BAMITA katika kutoa Elimu kwa
Jamii juu ya kupunguza maambukizi ya Ukimwi na Kudhibiti Mimba kabla ya
Ndoa.
Katibu
Mkuu wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA) ,Sheikh Salum Sung’he
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo picha) wakati akitoa shukrani
zake kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward
Lowassa,mara baada ya kuwakabidhi msaada wa shilingi mil. 5 kwa ajili ya
kuendeleza mipango kazi wa BAMITA katika kutoa Elimu kwa Jamii juu ya
kupunguza maambukizi ya Ukimwi na Kudhibiti Mimba kabla ya
Ndoa.Makabidhiano hayo yamefanyika leo Ofisini kwake jijini Dar es
Salaam.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Misikiti Tanzania
(BAMITA),Alhaj Juma Swalehe.
Katibu
Mkuu wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA) ,Sheikh Salum Sung’he
akikabidhi kwa Mh. Lowassa barua ya shukrani kutoka Baraza la Misikiti
Tanzania (BAMITA).Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Misikiti
Tanzania (BAMITA),Alhaj Juma Swalehe.