Kamanda wa polisi Mkoani Ruvuma Deusdedit Nsimek akizishika nyara za serikali hizo ambazo zimekamatwa(mikia ya tembo)
..................................................................................................
JESHI la polisi mkoani Ruvuma linamshikilia mtu mmoja ajulikanae kwa
jina la Bakari Said [17]mkazi wa kijiji cha mbalakiwa kata ya Ligunga
wilaya ya Tunduru mkoani humo kwa tuhuma ya kukutwa na mikia 10 ya Tembo
ambayo ni nyara za serikali huku ikikadiliwa kuwa na thamani ya shilingi milioni 247.
Akiongea
na waandishi wa habari ofisini kwake leo kamanda wa polisi wa mkoa wa
Ruvuma Deusdedit Nsimek amesema kuwa tukio hilo la kumkamata mtuhumiwa
huyo lilifanyika April 5 mwaka huu majira ya saa 7.15 usiku kwenye
Nyumba anayoishi mtuhumiwa huyo katika kijiji cha mbalakiwa baada ya
kupata taarifa kutoka kwa raia wema wa kijiji hicho.
Kamanda
amesema kuwa kumekuwepo kwa vitendo vya kijangili dhidi ya nyara za
serikali kwa majangili hao kuuwa wanyama mbalimbali hasa Tembo na
kuchukua pembe zao kwa malengo ya kwenda kufanya biashara kinyume na
taratibu za kisheria .
Amesema
kuwa licha ya mtuhumiwa huyo kutambuliwa akiwa na umri wa miaka 17
lakini sheria itachukua mkondo wake ilikubaini na wengine wanaofanya
vitendo hivyo .
“Kwa hali hii niwazi kuwa Tembo 10 wamepotea kwa kuuwawa pamoja
pembe zake 20 jambo ambalo limeisababishia hasara serikali kiasi cha
fedha kilicho kadiliwa kuwa ni shilingi milioni 247kwa fedha ya
kitanzania’alisema Kamanda huyo.
Aidha
kamanda amesema kuwa mtuhumiwa tayari anatarajiwa kufikishwa mahakamani
ili kujibu shistaka linalo mkabili na kuwa aliwaomba wananchi kuendelea
kushirikiana na jeshi la polisi kuwafichua watu wanaofanya vitendo
hivyo vya kulihujumu taifa.
MWISHO.