Hapa ni stendi ya daladala ziendazo Luwiko, Namanditi na Lilambo gari likiwa tupu kufuatia mgomo wa madereva .
Na Amon Mtega, Songea.
MADEREVA wa gari za abiria maarufu kwa jina la daladala
zinazofanya safari katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma
LEO wamegoma kutoa huduma kwa muda zaidi ya masaa mtatu kufuatia baadhi ya madereva
kunyang’anywa leseni ,kutolewa namba za magari hayo pamoja kubadilishwa
kwa vituo vya kupakia na kushusha abiria.
Tukio hilo limetokea
jana katika kituo cha daladala kilichopo maeneo ya Ikweta katika manispaa hiyo
na kusababisha usumbufu kwa abiria ambao walikuwa ndani ya daladala hizo kushindwa
kusafiri kwa kulazimishwa kushuka kabla ya safari zao na kumfanya mkuu wa
wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti pamoja
na timu yake kuingilia kati kumaliza
mgogoro huo.
Madereva hao
wakimueleza mkuu wa wilaya kufuatia mgomo huo
walisema kuwa waliamua kugoma kufuatia baadhi ya madereva wenzao
kunga’anywa leseni ,kutolewa namba ya gari,kunyanyashwa na baadhi ya askari
polisi wa usalama barabarani kwa kuzabwa vibao pamoja kubadilisha baadhi ya
vituo vya daladala hizo.
Kwa upande wake
kaimu mkuu wa mkoa wa Ruvuma ambaye pia
ni mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti akitatua mgomo huo aliwataka madereva hao waendelee na kazi ya utoaji wa
huduma ya usafirishaji abiria kwa kufuata sheria zinazo takiwa huku aliondoka
na viongozi wa madereva hao kwenda kujadili suala hilo kwa pamoja.
Akiongea na viongozi
wao katika ukumbi wa ofisi yake kaimu
mkuu wa mkoa huo alisema kuwa hakuna sababu za kufanya mgomo kwa kuwa
sheria za usalama barabarani zipo na zinatakiwa zifuatwe bila shuluti na
kuangalia vituo vilivyo kataliwa askari wa usalama maana vituo hivyo havipo
maeneno salama.
“Kitendo mnacho
dai kuwa mnanyanyaswa kwa kupigwa na kunyang’anywa leseni litaangaliwa kwa
kulifanyia kazi lakini kilichopo ni kuhakikisha leseni zenu ziwe zenye sifa ya
kubeba abiria “alisema mkuu huyo.
Naye kamanda wa
polisi wa mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki alisema kuwa yeye anafuata sheria ni
lazima sheria za usalama barabarani
zifuatwe na kuwa kama kuna askari usalama
barabarani anapokea rushwa kutoka kwa madereva hao basi sheria ichukue mkondo
wake .
MWISHO.